Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji Rufaa (mst) Semistocles Kaijage leo amefungua mkutano wa Watendaji wa Uchaguzi Mkoa wa Dar es Salaam. Jaji Kaijage amewataka watendaji hao kuepuka kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha kwamba kwenye Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani utakaofanyika tarehe 28 Oktoba 2020, Sheria, Kanuni na Taratibu zinafuatwa.
Mkutano huo uliwaleta pamoja Mratibu wa Uchaguzi wa Mkoa, Maafisa Uchaguzi, Wasimamizi wa Uchaguzi ngazi ya majimbo na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi ngazi ya Kata. Mkutano kama huo umefanyika kwenye vituo saba (7) nchi nzima.
0 comments:
Post a Comment