METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 17, 2020

TAWA KUNUFAIKA NA UWINDAJI WA KITALII


Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA   Imani Nkuwi Akizungumza na Rais  mstaafu kutoka The safari club international ya Nchini Marekani, Steve skold.

Meneja wa Pori la Akiba la Moyowosi Bigiramungu Kagoma akizungumzia kuimarika kwa mazingira ya pori  hilo.

MAMLAKA ya usimamizi ya wanyamapori Tanzania TAWA na rais mstaafu wa club kubwa ya uwindaji wa kitalii duniani Steve Skold wamekubaliana kushirikiana katika kuitangaza Tanzania kuwa eneo bora la uwindaji wa kitalii.

Hayo yamebainika Mara baada ya Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA   Imani Nkuwi kukutana na kufanya mazungumzo na Rais huyo mstaafu kutoka The safari club international ya Nchini Marekani, Steve skold.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika pori la Akiba la Moyowosi lilopo Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma ambapo Rais huyo mstaafu amekuja kufanya uwindaji wa kitalii mara baada ya kumaliza kipindi chake cha uongozi mwaka 2019 akiwa ameambatana muwindaji maarufu wa kitalii

Klabu hiyo kubwa duniani ina  wanachama zaidi ya 50,000 na matawi 200 ndani ya Marekani na 106 nje ya Marekani.

Mazungumzo hayo yamelenga kutumia fursa ya ujio wa Rais Mstaafu wa Safari Club International kutangaza utalii wa uwindaji nchini.

Aidha, Bwana Steve alifanya mahojiano maalum baadhi ya vyombo vya habari nchini ambayo na kueleza kuwa Tanzania ni  sehemu bora ya kufanya uwindaji wa kitalii katika mazingira halisi ( natural habitat) yenye bioanuai nyingi za maua, wadudu na ndege wemgi na wazuri.

Safar Club International Kila january hada february ya kila mwaka huandaa maonyesho makubwa ya uwindajiduniani ambayo yanahudhuriwa  na waonyeshaji zaidi ya 650,000 hivyo ni fursa nzuri kwa nchi ya Tanzania kuzidi kutangaza utalii huo wa kiwindaji.

Kwa upande wake Naibu kamishna Nkuwi alisema nchi ya Marekani kwa zaidi ya miaka 10 imekuwa iliongoza kwa asilimia 65 hadi 70 kwa wananchi wake kufanya utalii wa uwindaji nchini na hivyo ndio soko kubwa la aina hiyo ya utalii.

Aidha amesema fursa hiyo muhimu ya kushirikiana na bwana Steve katika kuwashawishi wamarekani kuwekeza katika kampuni za kuendesha utalii wa uwindaji ( hunting outfitters) na kuwaleta wamarekani wengi zaidi.

Pia Naibu Kamishna wa Uhifadhi (Utalii na Huduma za Biashara wa Mamlaka ya usimamizi wa wanyamapori Tanzania TAWA   Imani Nkuwi ameitaka jamii kujiepusha na vitendo kijangili jambo ambalo litaisaidia kupata  maendeleo.

Nae meneja wa Pori la Akiba la Moyowosi Bigiramungu Kagoma amesema kuwa mazingira ya pori hilo yanazidi kuimarika,

Bigiramungu ameongeza kuwa eneo hilo ni muhimu pia katika uwindaji hivyo kuwataka wananchi kuhakisha wanahifadhi rasiliamli hiyo muhimu kwa maendeleo yao.

Mmoja wa wawekeza katika Pori Hilo Adam Clements amesema kuwa hivi sasa wanampango wa kuisaidia jamii inayoishi pembezoni mwa kitalu hicho katika sekta ya elimu,ikiwemo kujenga madarasa,pamoja na madawati ili iweze kujiepusha na vitendo vya kijangili.

Adam amesema kuwa wanaamini kwa kufanya hivyo jamii inayozunguka eneo hilo watajua umuhimu wa uwindaji wa kitalii,pamoja na faida za wanyamapori katika maeneo yao.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com