METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 28, 2020

SUBIRA MGALU AENDELEA NA ZIARA YA KUOMBA KURA ZA CCM KATA KWA KATA


Mgombea Ubunge Mteule wa Viti Maalumu Mkoa wa Pwani (CCM) Bi,Subira Mgalu leo tarehe 28 Septemba 2020 ameshiriki ziara ya  kampeni ya Kata kwa Kata  pamoja na Kamati ya Utekelezaji ya Mkoa wa Pwani katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani ambapo amezungumza na Kamati za Ushindi za kata ya Ikwiriri ,Umwe na Mgomba Kumuombea  kura Mgombea Urais (CCM) Dkt John Pombe Magufuli,Mgombea Ubunge wa Jimbo la Rufiji (CCM) Ndugu Mohamedi Mchengerwa  pamoja na wagombea Udiwani kupitia Chama Cha Mapinduzi Ndugu Ally Ndungutu wa Kata ya Ikwiriri, Ndugu Muharami Mchambwa  Kata ya Umwe na Ndugu Omary Ndembo Kata ya Mgomba.

Mpaka sasa Kamati ya utekelezaji ya Mkoa pamoja na Wagombea Ubunge wameshafanya Mikutano ya Kuomba kura za CCM katika majimbo ya Bagamoyo , Chalinze , Kibaha Vijijini , Kisarawe na Mkuranga.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com