METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, May 13, 2026

SERIKALI KUENDELEA KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA WATUMISHI WA UMMA


Na. Antonia Mbwambo, Arusha.

Watumishi wa Umma nchini wamehakikishiwa kuboreshewa mazingira ya kazi kadri uchumi utakavyoruhusu ili kuleta tija katika utendaji kazi kwa maslahi ya umma.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Qwaray wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi Duniani yaliyofanyika leo tarehe 12 Mei, 2026 katika ukumbi wa AICC Jijini Arusha.

Mhe. Qwaray amesema, Serikali inatambua na kuthamini mchango wa Watumishi wa Umma wote nchini wakiwemo Wauguzi, hivyo itazingatia changamoto wanazokutana nazo watumishi hao, pamoja na kushughulikia kwa uzito unaostahili ili kutengeneza mazingira mazuri ya utendaji kazi. "Niwahakikishie Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya kazi na maslahi ya Watumishi wa Umma kadri uchumi utakavyoruhusu kwani tunatambua mchango wenu mkubwa katika kuwahudumia Watanzania, fanyeni kazi, Serikali ipo nanyi." Mhe. Qwaray alisema.

Aidha Mhe. Qwaray ameongeza kuwa, ili kuwa na ufanisi mkubwa katika utoaji wa huduma kwa wananchi Serikali itaendelea kuisimamia sekta ya afya pamoja na kuimarisha ushirikiano wa kitaaluma bila kuathiri misingi ya Utumishi wa Umma, Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ikiwemo uzingatiaji wa maadili.

Aidha amewataka kuwa na kauli nzuri, huruma na upendo utakaoongeza tija katika utendaji kazi ili kuleta mabadiliko chanya katika Sekta ya afya.

Ninyi ndiyo watu wa kwanza kukutana na mgonjwa pindi anapofika hospitali na ni watu wa mwisho mgonjwa anapotoka hospitali baada ya matibabu, ikiwa mtakuwa na nyuso za ukatili na ulimi mkali au wa kebehi, mtawakwaza wagonjwa na hata kuwakatisha tamaa jambo ambalo litaonyesha mapungufu katika sekta ya afya.”Mhe. Qwaray alisema.

Vilevile, Mhe. Qwaray amewaahidi Wauguzi hao kuwa Ofisi imepokea masuala yote waliyoyaeleza katika risala yao na kuwaahidi kuyawasilisha kwa ajili ya kufanyiwa kazi ikiwemo masuala ya Muundo Mpya wa Utumishi wa Kada ya Uuguzi na Ukunga na Muundo wa Utawala katika Sekta ya Afya ili kuboresha huduma ya afya na maslahi ya watumishi wa afya nchini. Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Qwaray, ametoa wito kwa wauguzi kuhahakisha wanabadili mienendo na tabia zisizopendeza wala kuendana na maadili ya kazi yao, lakini pia amewapongeza kwa jitihada kubwa wanazozifanya katika kuwahudumia wananchi na kuboresha afya zao.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Wauguzi (TANNA), Dkt. Ezekiel Mbao amemshukuru Naibu Waziri, Mhe. Regina Qwaray kwa kujumuika nao kwenye maadhimisho ya siku hiyo adhimu.

Maadhimisho hayo ya Siku ya Wauguzi Duniani yamebeba kauli mbiu isemayo Wauguzi Wetu, Mustakabali Wetu, Wauguzi Waliowezeshwa Huokoa Maisha.

Share:

1 comment:

  1. Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.

    Mume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
    Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
    Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.

    Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
    Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
    Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
    Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
    Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
    Nitaendelea kushukuru milele.
    Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
    . Usaidizi wa kurejesha ndoa
    . Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
    . Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
    . Mwongozo na ulinzi wa kiroho
    Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159. dawnacuna314@gmail.com

    ReplyDelete

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com