Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamnhuri Wiliam akitoa majizo kwa watendaji wa wilaya hiyo kuzingatia mafunzo waliyopewa juu ya kukabiliana na janga la moto
Picha ya pamoja ya baadhi ya watendaji wa wilaya ya Mufindi na Viongozi kutoka shamba la miti Sao Hill
Afisa zimamoto akitoa elimu kwa watendaji juu ya madhara ya moto katika msitu wa Sao Hill
Na Fredy Mgunda,Mufindi.
Wakala wa misitu Tanzania TFS kupitia shamba la Sao hill na Serikali ya Wilaya ya Mufindi wameanza kutoa elimu kwa maafisa watendaji wa kata na Tarafa juu ya ulinzi wa maeneo ya msitu na hasa juu ya kukabiliana na janga la moto unaozuka kutokana na shughuli za kibinaadam na kuteketeza msitu kila mwaka.
Akizungumza wakati Warsha maalum kwa ajili ya kukabiliana na moto inayoteketeza misitu katika wilaya ya Mufindi,Mhifadhi mkuu wa Shamba la Miti la Serikali Sao Hill Juma Mwita alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea viongozi uwezo wa elimu ya kukabiliana na janga la moto
“Kulingana na hasara inayojitokeza mara kwa mara awamu hii Wakala wa misitu Tanzania TFS pamoja na Serikali wameona ni vyema kuweka msisitizo katika kuwajengea uwezo watendaji wa kata na tarafa juu mbinu shirikishi za tahadhari ya kuzuka kwa mioto na namna ya kukabiliana nayo ili kuunusuru msitu wa sao hill na mashamba ya miti ya wananchi wilayani Mufindi” alisema Mwita
Mwita alisema kuwa mpango wa elimu shirikishi kwa viongozi na wananchi ni endelevu na wanataraji kupata matokeo chanya kutokana na mikakati iliyopo kwa viongozi hao kwenda kwa wananchi wanaowaongoza.
Aidha Mwita alisema kuwa Kando ya moto unaoteketeza misitu kila mwaka uvamizi katika maeneo ya shamba la miti la serikali sao hill ni changamoto nyingine ambayo inatakiwa kufanyiwa kazi ili kumaliza kabisa changamoto hizo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamnhuri Wiliam ametoa siku kumi na nne kwa maafisa tarafa ya Malangali na Saadani kuwasilisha ofisini kwake taarifa ya bank Ardhi iliyopo katika maeneo yao ili kuwapatia wananchi waliondoka katika maeneo vamizi ya hifadhi ya msitu wa Sao hill.
Jamhuri William ametoa agizo hilo kufuatia wananchi zaidi ya 60 waliovamia msitu huo kuridhia takwa la kuyaachia maeneo hayo ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuendelea kuyatunza maeneo ya hifadhi ya msitu huo unaotajwa kuchangia pakubwa ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo pamoja na pato la Taifa.
Jamhuri alitumia Warsha hiyo kueleza hatari ya moto inavyoweza kudumaza maendeleo yatokanayo na misitu
Hata hivyo ameonesha kutofurahishwa na maagizo aliyoyatoa dhidi ya afisa tarafa ya malangali juu ya benki ardhi ili kuwapatia wananchi waliovamia ardhi iliyo chini ya hifadhi ya msitu wa Sao hill na sasa anatoa maagizo
Msitu wa kupandwa wa sao hill ulio mkubwa kuliko yote afrika mashariki kando ya kuchangia pato la taifa umekuwa mhimili wa uchumi wa wilaya ya mufindi ukifungua fursa ya ajira kwa wananchi kuajiriwa katika kazi za uhifadhi lakini pia umefungua fursa kubwa ya kiuchumi kwa wananchi kujihusisha na kilimo pamoja na biashara ya mazao ya misitu.
0 comments:
Post a Comment