Dkt. Abbasi ameyasema hayo jana Jijini Dodoma alipokuwa
akifunga Mafunzo ya siku tatu yaliyotolewa kwa watumishi hao wa kada ya Habari
ikiwa ni tararibu ambazo hufanya kwa kila mwajiriwa mpya wa serikali.
"Natoa rai kwenu hakikisheni mnayaishi na kuyatenda
yale yote mliyofundishwa na Wataalamu ili muweze kutekeleza majukumu na kufikia
malengo yaliyowekwa na Serikali" Dkt.Abbasi.
Aliongeza kwa kueleza kuwa Wizara hiyo inasimamia sekta za
burudani ambazo huwaleta wananchi kwa pamoja na umoja bila kujali kabila wala
dini ambapo ni soft power muhimu ya nchi
hivyo watumishi hao walisisitizwa
kuzingatia utaalamu, weledi na ufanisi wakati wa kutekeleza majukumu yao ili kuleta manufaa kwa Serikali na
wananchi kwa ujumla.
Aidha Dkt. Abbasi aliwataka watumishi hao kuwa mabalozi
wazuri katika kutunza siri za serikali , kufanya kazi kwa ushirikiano, kuwa na
mahusiano mazuri na watumishi wengine,
kuweka malengo katika utendaji wao wa kazi ndani na nje ya utumishi wa
umma ili kuwezesha kufikia malengo yaliyowekwa na Wizara.
Mafunzo hayo yalihitimishwa
kwa kiapo cha uadilifu kwa watumishi wa umma ambacho waliapa mbele ya
mwajiri wao ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Hassan Abbasi.
0 comments:
Post a Comment