Serikali ya
Rais, Dkt. John Pombe Magufuli imetoa kiasi cha Dola za Marekani milioni 35.3 sawa
na bilioni 78 fedha Kitanzania kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kudhibiti
Sumukuvu nchini (Tanzania Prevention for Afflatoxin Contamination - TANPAC).
Sumukuvu
inatokana na fangasi wanaoota kwenye mazao ya chakula hususan mahindi na
karanga, ambapo fedha hizo zitatumika kujenga miundombinu mbalimbali, ikiwemo
maghala katika Halmashauri 14 Tanzania Bara na Zanzibar.
Akizungumza
kabla ya kutembelea eneo litakalojengwa ghala la kuhifadhia mazao ya chakula
katika kijijini cha Ikindilo wilayani Itilima mkoani Simiyu, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Kilimo, Bwana Gerald Kusaya anasema fedha hizo zitatumika kujenga
maabara mahususi ya kilimo Jijini, Dodoma; Kituo cha karantini ya utafiti wa
Sumukuvu, Kibaha mkoani Pwani pamoja na Kituo mahili cha mazao eneo la Mtanana,
mkoani Dodoma.
Aidha,
Katibu Mkuu Kusaya amesema kupitia mradi wa TANPAC Serikali itajenga Maghala 14
kwa ajili ya kuhifadhi mazao ya chakula aina ya nafaka na kutumia fursa hiyo
kuziomba Halmashauri hizo 12 (Tanzania Bara) na mbili Zanzibar kutoa maeneo
ambayo hayatakuwa na migogoro ya ardhi ili maghala hayo yajengwe mara moja.
Katibu Mkuu
Kusaya ameongeza kuwa thamani ya kila ghala, litakalojengwa katika Halmashuri
kila Halmashauri; Litagharimu kiasi cha shilingi milioni 480 na kuongeza kuwa
Serikali ya Awamu ya Tano imedhamiria kumkomboa Mkulima kutokana na changamoto
ya sumukuvu ambayo ina athari kubwa kwa afya za walaji pamoja na biashara ya
mazao ya kilimo ndani na nje ya nchi.
“Nawaomba Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya, Wakulima na Wananchi ambao Halmashauri zao zimepata fursa ya kujengewa maghala haya, waridhie na wataoe maeneo ambayo hayana migogoro ili mwezi Disemba, 2020 tuanze ujenzi, fedha ipo tayari na mchakato wa kuwapata Wazabuni upo kwenye hatua ya mwisho.” Amekaririwa Katibu Mkuu Kilimo, Bwana Gerald Kusaya.
0 comments:
Post a Comment