Na George Binagi-GB Pazzo
Serikali ya
Ireland imepongeza juhudi za kupambana na Ukatili wa Kijinsia katika
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, na kuahidi ushirikiano zaidi
ikiwemo kuendelea kufadhili miradi mbalimbali wilayani humo.
Mkuu wa
Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, Adrian Fitzgerald
aliyasema hayo kwenye mdahalo wa kupinga viashiria vyote vya ukatili wa
kijinsia kwa watoto na wanawake uliofanyika Kata ya Igokelo wilayani Misungwi.
“Nimefurahi
kuona fedha za walipa kodi wa Ireland zinatumika vizuri hapa Misungwi hivyo
serikali ya Ireland itaendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania kwa
kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo hapa Misungwi”. Alisema
Fitzgerald.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya Misungwi, Katibu Katawala wilayani humo Petro
Sabatho alisema Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya hiyo haitamvumilia yeyote
atakayejihusisha na ukatili wa kijinsia hususani mimba na ndoa za utotoni kuwataka
wazazi kufichua taarifa za aina hiyo ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Mkurugenzi Mtendaji
wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema wilaya ya Misungwi imekuwa wilaya
ya mfano kwa kutekeleza vyema mkakati wa kupambana na ukatili wa kijinsia na
hivyo kuwapongeza wanaharakati, madiwani pamoja na watendaji mbalimbali kwa
ushirikiano wao.
Halmashauri
ya wilaya Misungwi kwa kushirikiana na shirika la kutetea haki za wasichana na
wanawake KVULINI la Jijini Mwanza inaendesha kampeni ya kupambana na Ukatili wa
Kijinsia kwa watoto na wanawake wilayani humo kwa ufadhili wa shirika la watu
wa Ireland (Irish Aid).
Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye mdahalo huo.
Mkuu wa Maendeleo kutoka Ubalozi wa Ireland nchini Tanzania, Adrian Fitzgerald
Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza, ACP. Jonathan Shanna alisema jeshi hilo halitasita kuwashughulikia wale wote wanaojihusisha na ukatili wa kijinsia hivyo wenye tabia hiyo waache mara moja.
Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Mwanza akiwasilisha salamu zake kwenye mdahalo huo
Katibu Katawala wilayani humo Petro Sabatho akizungumza kwenye mdahalo huo na kuonya baadhi ya waalimu kuacha tabia ya kujihusisha na vitendo vya mahusiano ya kimapenzi na wanafunzi na kwamba sheria kali zitachukuliwa kwa yeyote atakayebainika.
Afisa Program shirika la Kivulini, Eunice Mayengelea akiongoza mdahalo huo
Watoto wakiwasilisha ujumbe wa kupambana na Ukatili wa Kijinsia kwa njia ya ngojera.
Tazama video hapa chini
0 comments:
Post a Comment