Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Henry Shekifu wakati alipowasili kwenye
uwanja wa Ndege wa Tanga kuanza ziara ya kazi mkoani humo, Oktoba 30,
2018. Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ametembelea eneo la mradi wa
ujenzi wa viwanda 11 katika kijiji cha Mtimbwani wilayani Mkinga, ambapo
amesema ameridhishwa na hatua za awali za uwekezaji huo.
Katika
eneo hilo vinatarajiwa kujengwa viwanda mbalimbali kikiwemo cha saruji cha
Hengya, kiwanda cha vioo, kiwanda cha vifaa vya kisasa vya ujenzi, uzalishaji
wa umeme kwa kutumia makaa ya mawe.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne, Oktoba 30, 2018) wakati akizungumza na
wananchi katika kijiji cha Mtimbwani wilayani Mkinga akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tanga.
Amesema
uwekezaji huo unatarajiwa kulinufaisha Taifa na wananchi wakazi wa wilaya ya
Mkinga kwa kuwa kinatarajiwa kuajiri zaidi ya watu 8,000, hivyo amewaomba
wananchi hao waendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji hao.
Kuhusu
wananchi ambao eneo lao limechukuliwa na wawekezaji na bado hawajalipwa fidia
Waziri Mkuu amewataka wawe na subira kwa kuwa wote watalipwa. “Muwekezaji
amenihakikishia kwamba atawalipa wananchi wote wanaodai fidia.”
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuuamewataka
watumishi wa umma kutenga siku tatu katika wiki na kuwafuata wananchi waishio
maeneo ya vijijini kwa ajili ya kusikiliza kero zao na kuzipatia ufumbuzi.
Amesema
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt. John Magufuli imedhamiria
kuwatumikia wananchi bila ya ubaguzi wa kidini, kisiasa,
rangi na kimapato, hivyo amewataka watumishi hao wafanye kazi kwa
bidii.
Awali, Mbunge wa jimbo la Mkinga, Dastan Kitandula ameishukuru Serikali kwa
niaba ya wananchi wa Mkinga baada ya Serikali kufuta hati ya shamba la moa na
kuirudisha ardhi hiyo kwa wananchi, pia ameomba ifute hayi za mashamba mengine
yaliyotekelezwa katika Tarafa ya Maramba.
0 comments:
Post a Comment