METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 1, 2020

MAKAMU WA RAIS AZITAKA WIZARA NA TAASISI KUKUTANA NA WADAU KUTATUA CHANGAMOTO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akikagua moja ya mabanda katika maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani Simiyu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Wananchi katika Viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu wakati wa Uzinduzi wà Maonesho ya Nane Nane.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara na Taasisi za Umma na binafsi kuwa mstari wa mbele kutafuta na kuwakutanisha wadau  wa sekta husika kujadili changamoto katika sekta husika.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema hayo leo Mkoani Simiyu wakati akizindua maonesho ya Kilimo, Mifugo na uvuvi Nane nane.

Ametaja baadhi ya changamoto zilizopo kuwa ni pamoja na miundombinu ya usafirishaji, upatikanaji wa mitaji, maeneo ya uwekezaji.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza majadiliano ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto yafanyike katika viwanja vyote vya maonyesho nchini ili kuhamasisha wananchi kushiriki kikamilifu na kunufaika na elimu inayotolewa.

Aidha, Makamu wa Rais, ameviagiza Vitengo na Idara za Mawasiliano Serikalini kushiriki kikamilifu kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu na manufaa ya maoñyesho yanayoendelea kote nchini.

Katika hatua nyjngine, Makamu wa Rais amewakumbusha Wananchi kushiriki katika uchaguzi Mkuu ujao unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

“Nayasema haya kwa kuzingatia kuwa maonesho ya Kilimo Nane Nane mwaka huu kauli mbiu yake inalenga kuwakumbusha Wakulima, wafugaji na wavuvi kote nchini kuchagua viongozi Bora” alisema

Hata hivyo, amewataka viongozi wa vyama vya siasa kufanya Kampeni kwa kuzingatia taratibu zinazotolewa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi vinginevyo, Serikali haitasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa wakakaofanya kampeni zinazolenga kujenga chuki na kuvuruga amani iliyopo.

Akizungumzia maoñesho yanayoendelea katika viwanja vya Nyakabindi, Mkoani Simiyu, 

Makamu wa Rais ameeleza kufurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Wizara za kisekta kwa kushirikiana na wadau mbalimbali zikiwemo taasisi za utafiti, mabenki na sekta binafsi.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com