METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 16, 2020

Mhe Mgumba Afanya ziara kukagua miradi ya maendeleo iliyopo chini ya Wizara ya Kilimo-Morogoro



Pichani Mhe Mgumba akikagua maendeleo ya uendelezaji wa shamba la miwa la Mkulazi holding Company Limited  Kampuni Tanzu ya NSSF.

Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mheshimiwa Omary Mgumba,amefanya ziara ya siku Mbili Mkoani Morogoro kukagua Miradi ya maendeleo iliyo chini ya wizara ya kilimo,ambapo katika ziara hiyo ameshuhudia mafanikio makubwa yanayofanywa katika miradi hiyo.

Mhe Mgumba amefika kukagua na kujionea maendeleo ya utayarishwaji wa vitalu vya miwa  ikiwemo Utayarishwji wa Kutalu ulioanza tangu mwezi ea Tatu mwaka huu na upandaji wa Kitalu cha miwa utaanza mwanzoni mwa mwezi wa 8 mwaka huu 2020.

Ambapo pia kwa sasa limelimwa eneo la hekta 200ha na kuanza kuoanda kitalu S cha 25ha na baada ya miezi sita kuhamishiwa kwenye kitalu B cha hekta 200ha na kuhamishiwa kwenye shamba kuu la mwanzo la hekta 5000ha.

Aidha pia Mhe Mgumba alifika kukagua Kiwanda cha mkulazi holding comoany Limired kitakachokuwa kikubwa kiliki vyote Afrika Mashariki na kati cha kuzalisha tani 200,000Mts kwa mwaka na kajiri watu zaidi ya laki moja (100000) kinajengwa kwenye kata ya mkulazi tarafs ya Ngerengere Jimbo la Morogoro kusini Mashariki Jimbo linaloongozwa na Mhe Mgumba Ambaye pia Naibu waziri wa kilimo.

Kiwanda hiki kinaendelea kuleta manufaa makubwa kwa wanachi wa Mkulazi, ngerengere Jimbo la Morogoro kusini Mashariki , Morogoro vijijini Mkoa wa Morogoro na Taifa kwa ujumla.

Aidha mradi huo unaendelea kuinarisha huduma za jamii kama vile barabara zikizoanza kurengezwa kutika Kwaba kwenda Usungura na Barabars ya ngerengere Kidunda itakayoanza kujengwa muda sio mrefu baada ya kupatikana fedha zilizotolewa na Mge Raisi na serikali Dkt Maguguli na serikali yake katika kurahisihda shughuli za maendeleo na uendelezaji wa shamba la miwa la Mkulazi kwa lengo la kuinua uchumi wa watu eneo hili pamoja na kumaliza tatizo ka sukari nchini.

Katika ziara hiyi Mhe Mgumba Aliambatana na Mkurugenzi mkuu wa Bodi ya Sukari Prof Bengesi, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF ndugu Erio, Mwenyekiti wa Bodi Ya mkulazi Holding Company Limited Dkt Msita, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa uchumi na fedha  wa  Morogoro Dkt Lozaria pamoja na viongizi wa chama na serikali wa wilaya, kata,vijiji na vitongoji wa mkulazi.

Manufaa mengine ya mradi huu ni ajira zilizoanza kupatikana katuka kuandaa shamab kwa watu wa Mkulazi, umeme ulioanza kupelekwa kuelekea eneo la mradi, maji , huduma za afya na elimu zinaendelea kuboreshwa kukidhi mahitaji ya wananchi na mradi.

Mhe Mgumba baada ya jumakiza ziara ya Morogoro vijijini ataendelea na kumalizia ziara yake wikyani kilosa siku ya alhamisi ya tarehe 16 Julai 2020.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com