Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina,
akizungumza wakati wa kufunga kikao cha Baraza la Madiwani.
Sehemu ya Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi
wakifuatilia Mjadala wa bajeti.
Na Afisa Habari Mufindi
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi limejadili, kuridhia na kupitisha rasimu ya bajeti yenye zaidi ya shilingi bilioni 62.926, ikiwa ni makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka ujao wa Fedha 2018/2019, ambapo makusanyo ya ndani ya Halmashauri ni Bilioni 4.162 kati ya Fedha zote.
Akiwasilisha rasimu ya bajeti
kwenye kikao maalum cha Baraza, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mufindi Bw. Isaya Mbeje, amesema, Halmashauri inatarajia kukusanya, kupokea na
kutumia zaidi ya Bilioni 62.926, ambapo kati ya Fedha hizo Bilioni 40.728 ni
Fedha kutoka Serikali kuu maalum kwa ajili ya mishahara ya Watumishi, Bilioni
17.205 zimeelekezwa kwenye Miradi ya Maendeleo huku Bilioni 4.992 ni kwa ajili
ya matumizi mengineyo.
Mbenje ambaye pia ndiye Afisa
Mipango wa Halmashauri, amevitaja vipaumbele vya bajeti hiyo kwa mwaka wa Fedha
wa 2018/2019 kuwa inaangazia ukamilishaji wa miradi ambayo haikukamilika kwa
miaka ya nyuma hususani ukamilishaji wa Majengo ya sekta ya Afya na Elimu,
Ukarabati wa Madarasa chakavu ya baadhi ya Shule za Msingi, ukusanyaji Mapato
kwa njia ya kielekroniki, Kutoa huduma bora za kijamii, kuinua uchumi wa
wananchi na kuimarisha Miundombinu.
”Mhe Mwenyekiti rasimu hii ya
Mpango wa Bajeti ya Halmashauri ni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka
2018/2019, rasimu hii itaendelea kujadiliwa na kupatiwa ushauri kwenye vikao
vya ngazi ya Mkoa, Ofisi ya Rais TAMISEMI Pamoja na Wizara ya Fedha na Mipango
kablaya kujadiliwa na kupitishwa na Bunge” libainisha Bw. Mbenje.
Azungumza wakati wa kufunga
kikao hicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi ambaye pia ndiye Diwani
wa kata ya Mninga Mhe. Festo Mgina, amewataka Madiwani kutoa ushirikiano kwenye
zoezi la ukusanyaji wa mapato pamoja na kubuni vyanzo vipya vya mapoto ili
yasaidie kuharakisha maendeleo kwa kuzingatia kuwa asilimia 60% Mapato ya ndani
yanatakiwa kuelekezwa kwenye miradi ya Maendeleo.
“Mkurugenzi wewe pamoja na
timu yako tuendelee kuchapa kazi, tunasifa ya Ushirikiano kati ya timu ya
Madiwani na Timu yako, tuendeleee kufanya kazi kwa umoja, uadilifu na
ushirikiano Kwani sisi kama Viongozi tunatakiwa kuwa chachu ya Maendeleo”
Rasimu ya bajeti ya 2018 –
2019, aimeandaliwa kwa kuzingatia, Ilani ya Chama cha tawala CCM, Mwongozo wa
bajeti wa mwaka 2018/2019, Mpango wa pili wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka
2016/2017, Malengo 17 ya maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment