Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) akifurahi jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini Mhe Dkt. Khamis Kigwangala mara baada ya kutembelea uliopokuwa mgodi wa Dhahabu wa Resolute katika kijiji cha Isanga kilichopo Kata ya Lusu Wilayani Nzega, Leo 26 Februari 2018. Picha Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini Mhe Dkt. Khamis Kigwangala wakikagua uliopokuwa mgodi wa Dhahabu wa Resolute katika kijiji cha Isanga kilichopo Kata ya Lusu Wilayani Nzega, Leo 26 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya ofisi za Kampasi ya Chuo cha Madini Dodoma (MRI) kwenye eneo lililokuwa mgodi wa Dhahabu wa Resolute katika kijiji cha Isanga kilichopo Kata ya Lusu Wilayani Nzega, Leo 26 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko pamoja na mwenyeji wake Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini Mhe Dkt. Khamis Kigwangala wakikagua uliopokuwa mgodi wa Dhahabu wa Resolute katika kijiji cha Isanga kilichopo Kata ya Lusu Wilayani Nzega, Leo 26 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Tabora
Serikali imebainisha kuwa zipo taarifa za maafisa wa serikali
waliopewa dhamana ya kusimamia sekta ya madini lakini wamekuwa kikwazo kwa kuwa
na usumbufu mkubwa wa manyanyaso kwa wachimbaji wadogo nchini.
Unyanyasaji huo unajili wakati ambapo wachimbaji hao wametumia
nguvu na muda wao mwingi na hatimaye kujipatia Madini lakini kabla ya kuuza
maafisa mbalimbali wa serikali hususani katika sekta ya Madini huingiza kikwazo
kwa madai ya kuhitaji mgao Mara baada ya mauzo.
Naibu Waziri wa Wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko
amesisitiza hayo wakati akiwa katika ziara za kikazi katika Mkoa wa Rukwa,
Katavi na Tabora ambapo amewataka maafisa hao kuacha Mara moja kadhia hiyo
kwanini kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu na sheria za utumishi wa
umma.
Leo 26 Februari 2018 akiwa katika Kijiji cha Isanga kilichopo
katika Kata ya Lusu Wilayani Nzega akizungumza na wananchi ambao asilimia kubwa
ni wachimbaji wadogo katika eneo ambalo ulikuwa mgodi wa Dhahabu wa
Resolute, Mhe Biteko aliwasihi wachimbaji hao kuwa wavumilivu wakati serikali
inafanya utaratibu bora katika sekta ya Madini ili kuwa na uchimbaji wenye
tija.
Mhe Biteko akiwa katika eneo hilo ambalo kwa sasa ni Kampasi ya
Chuo cha Madini Dodoma (MRI) alisema kuwa serikali haitatoa ruzuku kwa wachimbaji
wadogo badala yake itatoa wataalamu na Vifaa vya Utafiti ili kubaini maeneo
yenye Madini na hatimaye wananchi kuchimba maeneo yenye uhakika wa rasilimali
hiyo.
Katika hatua nyingine rungu limewaangukia Wamilili wa
Leseni za Madini ambao hawajayaendeleza maeneo yao ambapo alisema kuwa serikali
inaendelea kujiridhisha pindi itakapomaliza ufuatiliaji wake itawaandikia hati
ya makosa kisha kuwafutia maeneo hayo kwa ajili ya kuwakabidhi wachimbaji
wadogo.
Kwa upande wake Waziri wa Maliasili na Utalii ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nzega Vijijini Mhe Dkt. Khamis Kigwangala amewahakikishia
wananchi wa jimbo hilo kuwa serikali ya awamu ya tano imekusudia kuwanufaisha
wananchi kupitia rasilimali mbalimbali ikiwemo madini hivyo ziara ya Naibu
Waziri Mhe Doto Mashaka Biteko nitakuwa na tija kwani amejionea uhitaji wa
maeneo kwa wachimbaji wadogo.
Aidha, aliwasisitiza Wachimbaji hao pindi serikali itakapotoa
ruhusa ya maeneo yao ya kuchimba kuzingatia Sheria na Taratibu ili kuwa na
uchimbaji wenye tija na uzalishaji mkubwa.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment