Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif
Ali Iddi, akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Ugeni wa
Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Walipomtembelea Ofisini kwake leo Juni 3, 2020 Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif
Ali Iddi, akifanya mazungumzo na Ugeni wa Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Haki
za Binadamu, Walipomtembelea Ofisini kwake leo Juni 3, 2020 Vuga Mjini
Zanzibar, kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Msataafu, Mathew
Mhina, Makamu Mwenyekiti, wa Tume ya
Haki za Biadamu na Utawala Bora, Mohamedi Khamis Hamadi, Kamishina wa Tume ya
Haki za Binadamu Zanzibar, Khatibu Mwinyi Chande na Kamishina wa Tume ya Haki
za Binadamu Tanzania Bara, Bi.Amina Talib Ali.
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif
Ali Iddi, akifafanua jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Ugeni wa
Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Walipomtembelea Ofisini kwake leo Juni 3, 2020 Vuga Mjini Zanzibar, Kulia
ni Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora,
Jaji Mstaafu Mathew Mhina
Makamu wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, akipokea kitabu
kinachohusu masuala ya haki za binadamu na utawala bora kutoka kwa Mwenyekiti
na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mhina, Walipomtembelea Ofisini kwake leo Juni 3, 2020
Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu
wa Pili wa Rais, Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi (wa kwanza kulia), akimsikiliza
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Mathew Mhina,
alipokuwa akizungumza katika ziara yake na Wajumbe wa Tume hiyo iliyoanza leo
Mjini Zanzibar, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Biadamu na
Utawala Bora, Mohamedi Khamis Hamadi.
Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi ameitaka Tume ya Haki za
Binadamu Tanzania kufanya wajibu wake wa kuwaelimisha wananchi kuhusu haki ili
kuelewa haki zao pindi wamapokuwa na matatizo mbalimbali ya kijamii kwa kufanya
kazi kwa karibu Serikali na kutekeleza majukumu yake kwa lengo la kuwatumikia
vyema Wananchi wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania.
Akizungumza
Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar alipotembelewa
na ujumbe wa Tume hiyo wakiongozwa na Mwanyekiti wake, Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina, alisema, Zanzibar imekuwa na
matukio mengi ya unyanyasaji wa kijinsia jambo ambalo Tume ya Haki za Binadamu
inapaswa kuwaelimisha wananchi kuhusu upatikanaji wa haki pamoja na wakuwaeleza
madhara ya unyanysaji wa kijinsia, kwani kufanya hivyo kutaisaidia Serikali kuu
kupata nguvu na uwezo wa ziada wa kutatua changamoto mbali mbali zinazowakabili
Wananchi hususan Wanawake, Watoto na hata Wananchi wenye mahitaji Maalum.
“ Tume ya
Haki za Binadamu ina kazi kubwa katika kutekeleza majukumu yake kwa upande wa Zanzibar kutokana na migogoro
na changamoto nyingi zinazowakabili Wananchi hali inayosababisha mitafaruki na
mifarakano miongoni mwa Jamii yenyewe, kwa hiyo nyie kama tume waelimisheni
wananchi wa Zanzibar kufahamu sehemu ya kupata haki zao, lakini pia nyie mna
jukumu kubwa la kusaidia kutatua migogoro na mifarakano inayotokea ya
wananchi kusumbuliwa katika maeneo tofauti Nchini ” Alisema Balozi
Seif .
Aidha ,
Balozi Seif aliueleza Uongozi wa Tume ya Haki za Binadamu kwamba yapo matatizo
mengi yanayowakabili Wananchi hasa Wanawake ya kupewa ovyo Talaka na matokeo
yake kutelekezwa na waume zao sambamba na kuachiwa watoto bila ya huduma hali ambayo inakuwa ni
kazi kwao kutimiza majuku ya kulea watoto.
Alitahadharisha
kwamba tabia hii iliyoanza kuota mizizi kwa baadhi ya Wanaume wasiojali utu wa
Binadamu ni ya hatari kwa Mtoto kwa vile inawakosesha haki zao za Msingi kama
vile kupata elimu na huduma za Afya kwa sababu ya kutokuwa na ushirikiano wa
kimalezi baina ya pande mbili.
Pia
alieleza suala la
udhalilishaji wa wanawake na watoto
linaloikumba Dunia, hivyo watendaji na Viongozi wa Tume ya Haki za
Binadamu lazima wajikite zaidi kushirikiana na Taasisi za utoaji haki pamoja na
Wananchi katika vita ya kukabiliana na tatizo hilo linalochangia kupotoshwa kwa
Maadili ya Jamii.
“Kwa sasa
masuala ya wanawake na watoto kudhalilishwa limekuwa ni jambo ambalo duniani
kote ni mtihani , kwa hiyo Tume ya Haki za Binadamu jikiteni zaidi katika
kufanya upembuzi wa suala hili, ili Taasisi za utoaji haki na Serikali ipate
kuwasaidia wananchi kupitia nyinyi, lakini pia misisahau kutoa elimu kuhusu
haki zao kwani hiyo pia itawasaidia kupambana na waharifu na wavunjaji wa haki
za Binadamu”, Alisema Balozi Seif.
Akijibu
ombi la Tume ya Haki za Binaadamu la
kupewa jengo la Ofisi kwa upande wa Zanzibar,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliushauri ujumbe wa Tume kuwa na
mpango wa kujenga majengo ya kudumu ya Ofisi zake Visiwani Zanzibar kwani
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iko tayari kutoa maeneo ya ujenzi huo wakati
wowote pale itapohitajika kutekelezwa mpango huo.
Kwa upande
wake, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za
Binadamu Tanzania Jaji Mstaafu Mathew Pauwa Mhina, alisema Taasisi hiyo ni
Chombo cha Umma kilichoundwa kusimamia upatikanaji wa Haki za Binadamu ili
kusimamia Utawala Bora hapa Nchini na kuwawezesha wananchi kupata haki zao za
msingi pale inapohitajika
“Tume ya haki za binadamu imeundwa na viongozi wake
waliteuliwa na Mhe Rais John Pombe Magufuli ili kutetea haki za Watanzania bila
kujali imani zao, kwa hiyo utekelezaji wa majukumu yake upo kwa ajili ya
wananchi wanaopokonywa haki zao, lakini pale ambapo watandaji wa Tume wakienda
tofauti ni masuala ya kibinadamu ya kuteleza
katika Utekelezaji wa majukumu yao, hivyo Viongozi Wakuu wanapaswa
kushauri pale Watendaji hao wanapoteleza katika maeneo yao ya Kazi”, Jaji
Mstaafu Mathew Mhina.
Aidha Tume
ya Haki za Binadamu Tanzania kupitia Mwenyekiti wake iliipongeza Serikali ya
Jamahuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi kubwa
inayoifanya ya kuhudumia wananchi jambo ambalo uongozi wa Tume hiyo
unaliunga mkono.
Makamishina
wa Tume ya Haki za Binadamu Tanzania waliteuliwa na Rais wa Jamuhuri ya
Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli mnamo Tarehe 19 Septemba Mwaka
2019, ili kuhakikisha kunakuwepo na upatikanaji wa haki kwa watanzania katika
maeneno yote ya Kijamii.
0 comments:
Post a Comment