Meneja Mkuu
wa Kampuni ya Gesi (GASCO) ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya
Petroli nchini( TPDC) Mhandi Baltazar Mroso( katikati) akitoa maelezo ya namna
ya gesi inavyosafirishwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said(
mwenye ushungi) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu huo ya kutembelea mradi wa gesi
asilia katika Mkoa wa Lindi na Mtwara, Mei 30- Juni 01,2020.
Meneja Mkuu
wa Kampuni ya Gesi (GASCO) ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika la Maendeleo ya
Petroli nchini( TPDC) Mhandi Baltazar Mroso( katikati) akimuonesha mita ya
kupima kiwango cha gesi asilia inayosafirishwa kupitia vituo vya usalama na
dharura vya kusafirisha gesi hiyo kwa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi
Zena Said( mwenye ushungi) wakati wa ziara ya Katibu Mkuu huo ya kutembelea
mradi wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na Mtwara, Mei 30- Juni
01,2020.Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.
Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said( mwenye ushungi) akishika bomba la
kusafirisha gesi alipotembelea kituo moja ya vituo vya usalama na dharura vya
kusafirisha gesi asilia wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa gesi asilia
katika mkoa wa lindi na mtwara, Mei 30- Juni 01,2020. Kushoto Viongozi
Waandamizi wa Wizara na Taasisi alioambatana nao katika ziara hiyo.
Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati, Mhandisi Zena Said( mwenye wa pili kulia) akitoa maelekezo
kwa msimamizi wa eneo linalochimbwa gesi asilia la Mnazi Bay, Msimbati
alipotembelea moja ya vituo vya usalama na dharura vya kusafirisha gesi asilia
wakati wa ziara yake ya kutembelea mradi wa gesi asilia katika Mkoa wa Lindi na
Mtwara, Mei 30- Juni 01,2020.
Mhandisi
Zena alifanya ziara hiyo mwishoni mwa juma kwa kukagua visima vya kuchimba gesi
vilivyopo Mnazi Bay eneo la Msimbati pamoja na Kiwanda cha Kuchakata Gesi hiyo
cha Madimba mkoani Mtwara na Kituo cha kupokea gesi na kufua Umeme cha Somanga
Fungu mkoani Lindi, Mei 30- Juni 01,2020.
Mhandisi
Zena alifanya ziara hiyo kwa lengo la kuona utendaji kazi wa mfumo mzima wa
uchimbaji, uchakataji, usafirishaji wa gesi asilia na kufua umeme pamoja na
matumizi mengine ya majumbani,mahotelini, viwandani na kwenye magari.
Baaada ya
kukagua na kuona ufanyaji kazi wa mfumo huo, alilipongeza Shirika la Maendeleo
ya Petroli nchini (TPDC) kwa kuendela kufanya kazi kwa weledi na uzalendo
mkubwa.
“Huu ni
mradi wetu sisi watanzania tunajivunia sana kuwa nao, hongereni sana TPDC
mnafanya kazi nzuri sana na inaonekana, watanzania pia wanafahamu juu ya kazi
yenu, uzalendo ndiyo kitu cha msingi kwa kila taifa ili liweze kuthamini vitu
vyake vya ndani na kusonga mbele, wataalamu simameni imara kwa maslahi mapana
ya taifa lenu, sisi serikali tunawapongeza sana” Alisema Mhandisi Zena.
Aliliagiza
shirika hilo, kuendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa wataalam wa
mradi huo ili kuwajengea uwezo zaidi wa kitaaluma ili kukabiliana na ukuaji
tekelolojia unaendelea kukuwa duniani kila siku.
Vilevile
alitoa wito kwa wataalamu hao kuwa wasikubali kurubiniwa kwa namna yeyote ile,
na kwa wale wakongwe na wenye uzoefu wa muda mrefu katika utekelezaji na
usimamizi mradi huo,wasiwe wanyimi bali wawarithishe uzoefu na ujuzi zaidi
vijana ambao ni wapya katika taaluma hiyo licha kuwa na elimu kubwa.
Kwa upande
wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini, (TPDC) Dkt.
James Mataragio alieleza kuwa mbali ya kuwepo kwa tishio la Virusi vya Corona
nchini, uzalishaji wa gesi asilia haukuathirika badala yake uliendelea kuongeza
kutoka futi za ujazo milioni siti hadi kufikia futi za ujazo milioni tisini.
“Corona
haikuathiri kabisa uchimbaji na uzalishaji wa gesi asilia hapa nchini,
tumeendelea kufanya kazi kwa kuchukuwa tahadhari, tukizingatia maelekezo ya Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Uzalishaji wa Gesi hadi kufikia Mwezi
Aprili mwaka huu 2020 ilifikia futi za ujazo milioni 90, na umeme unaozalishwa
sasa unatumia gesi hiyo pamoja na ule unaotokana na vyanzo vya maji”, Alisema
Dkt. Mataragio.
Hii ni mara
ya kwanza kwa Katibu Mkuu huyo wa Wizara ya Nishati kutembelea mradi huo wa
gesi, baada ya kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo mapema mwaka huu.
Katibu Mkuu
huyo pamoja na ujumbe wake, pia walitembelea kiwanda cha kutengeneza Malumalu
pamoja na Mabox cha GodWill kilichopo wilayani Mkuranga mkoani Pwani
kinachotumia gesi asilia inayochimbwa hapa nchini kufanya shughuli zake za
uzalishaji.
0 comments:
Post a Comment