METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, March 23, 2020

KILOMITA 39 ZA LAMI ZAANZA KUJENGWA MJI WA SERIKALI MTUMBA DODOMA

Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe akionesha kazi ya ujenzi wa barabara za lami inavyoendelea
Eneo lililosafishwa tayari kwa ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Ujenzi wa barabara za lami katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma waanza kwa kasi ili kuimarisha mawasiliano na huduma kwa wananchi.

Akizungumza leo Machi 20, 2020 katika mahojiano maalum, Katibu wa Kikosi Kazi cha Taifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali kuhamia Dodoma Bw. Meshack Bandawe amesema kuwa ujenzi huo unahusisha barabara zenye urefu wa kilomita 39 ndani ya mji huo.

“Serikali inaimarisha miundombinu ndani ya mji wa Serikali ikiwemo ujenzi wa barabara za njia mbili zenye urefu wa kilomita 28 na zenye njia 4 kilomita 11, ujenzi huu unaenda sambamba na kujengwa kwa miundombinu mingine kama TEHAMA, Afya,Makazi na Sehemu za Biashara”, Alisisitiza Bandawe Akifafanua Bandawe amesema kuwa ujenzi wa miundombinu katika mji wa Serikaliunaenda sambamba kujengwa kwa majengo ya gorofa kwa ajili ya matumizi ya Ofisi
za Wizara 22.

Mji wa Serikali ulizinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mwezi Machi 2019.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com