Rais Jajaya Mrisho Kikwete akiongea na Watanznia wanaoishi India
katika Hotel ya Taj Palace jijini Delhi. Rais Kikwete aliwaeleza mambo
ya maendeleo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya nne ikiwemo ujenzi wa
miundombinu kama vile barabara, maji, umeme na uboreshaji wa bandari ya
Dar es Salaam. Aidha, aliwambia mipango iliyopo ya kujenga bandari ya
Bagamoyo na reli ya kati ya kisasa. Aliwaeleza pia hali ya kisiasa,
hususan maandalizi ya uchguzi mkuu ambapo zoezi la kuchukua fomu za
kuwania nafasi ya Rais linaendelea.
Baadhi ya Watanzania waliohudhuria mkutano wa Rais Kikwete
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (Mb) kulia na Naibu Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb)
nao waliongozana na Rais Kikwete katika mkutano na Watanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekzaji Tanzania (TIC), Bi. Juliet
Kairuki akitoa ufafanuzi wa masuala ya uwekezaji kwa Watanzania
wanaoishi India.
Dada wa Kitanzania ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa Shahada ya
Uzamili ya masuala ya Teknolojia ya Kilimo nchini India akimuuliza swali
Rais Kikwete. Dada huyo alitaka kujua Serikali imejipngaje kuhakikisha
kuwa mazao yanayolimwa nchini Tanzania yanasindikwa kabla ya
kusafirishwa nje ya nchi. Rais Kikwete alieleza kuwa katika awamu ya
pili ya mpango wa maendeleo wa mwaka 2025 ambao unaanza kutekelezwa
mwaka 2015/2016 unalenga maendeleo ya viwanda.
Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa wafanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini India.
Rais Kikwete (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Me. Mhandisi John Kijazi
Mama Salma Kikwete (katikati) akiwa na baadhi ya Watanzania wanawake wanaoishi India.
Picha kwa hisani ya Wizara ya Mambo ya Nje
0 comments:
Post a Comment