Waziri wa Madini Doto Biteko akiwa na Mkurugenzi wa PRNG Lucas Stanfield kulia ofisini kwake jijini Dodoma.
Waziri wa Madini Doto Biteko amesema utaratibu wa upatikanaji wa leseni za madini za aina mbalimbali hupatikana kwa mujibu wa sheria na taratibu. Amesema, sheria hizo hutumika kulinda leseni hizo ili ziwe hai. Kwa kuzingatia masherti yaliyomo kwenye leseni, atakayeshindwa kuzingatia
masherti hayo sheria hutumika ikiwemo kutoa hati ya makosa (default notes) na hatimae kuzifuta.
Biteko ameyasema hayo leo tarehe 6/02/2020 wakati wa kikao chake na kampuni ya Peak Resources Ngwala (PRNG) ofisini kwake jijini Dodoma akizungumzia masuala ya utoaji wa leseni za uchimbaji madini. PRNG walikuwa wakifuatilia upatikanaji wa leseni ya uchimbaji madini ambapo
Biteko amesema suala lao linashugulikiwa na taratibu zikikamilika watapatiwa.
Amesema wakati wa sasa suala la leseni siyo kificho na halihitaji kumuona mtu ili upate leseni, kubwa ni kufuata utaratibu uliowekwa na kuzingatia sheria. Ameongeza kuwa leseni ya PRNG ikikamilika itatolewa. Mkurugenzi wa PRNG Luca Stanfield amemshukuru waziri kwa mazungumzo yake huku wakisema wanachosubiri kupata leseni ili waanze kazi na watafwata sheria.
Biteko amesema leseni zinatolewa kwa kila mtu iwe wa ndani au nje ya nchi anapaswa kuzingatia sheria na taratibu. “Kwenye utoaji wa leseni kuna sheria za kuzingatia ikiwemo ulipaji tozo za kodi za serikali ambazo muombaji anapaswa kuzifahamu na kulipa” amesema Biteko.
0 comments:
Post a Comment