Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena akifafanua jambo kwa
Waandishi wa Habari (hawapo pichani), katika hafla fupi ya kupewa Ubalozi wa
Utalii wa Tanzania nchini Uingereza kwa bwana Nick Reynald ‘Bongozozo’ iliyofanyika
Jijini Dar es Salaam, leo Februari 04, 2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB,
Geofrey Tengeneza na kushoto ni Balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania nchini
Uingereza, Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’
Balozi wa hiari wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza, Bw. Nick Reynald
‘Bongozozo’ akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), katika
hafla fupi ya kupewa Ubalozi wa Utalii wa Tanzania nchini Uingereza
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, leo Februari 04, 2020, kulia ni Afisa Uhisiano
Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza na kushoto ni Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii
(TTB), Geofrey Meena
Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena(kushoto) akimkabidhi
jarida la utalii (Tanzania Unforgetable) Bw. Nick Reynald ‘Bongozozo’(katikati)
aliyekabishiwa barua rasmi kuwa balozi wa
hiari wa utalii wa Tanzania nchini Uingereza,
kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey Tengeneza
Meneja Masoko kutoka Bodi ya Utalii (TTB), Geofrey Meena(kushoto) akimkabidhi
FLASH yenye video za utalii wa
Tanzania
balozi wa hiari wa utalii wa
Tanzania
Bw.Nick Reynald
‘Bongozozo’(katikati)
aliyekabishiwa
barua rasmi leo Februari 04,2020, kulia ni Afisa Uhisiano Mkuu TTB, Geofrey
Tengeneza.
Wizara ya
Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii nchini (TTB), leo imetekeleza agizo
la Waziri wa Wizara hiyo, Dkt.Hamisi Kingwala alilolitoa Jijini Dodoma jana
Februari 03,2020 la kumpa Mwingireza Nick Reynald maarufu kama Bongozozo
ubalozi wa utalii wa Tanzania nchini Uingireza.
Akizungumza
katika hafla ya kumkabidhi barua ya utambuzi kwa ajili ya kazi hiyo
iliyofanyika Jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa TTB, Geofrey Meena alisema
kuwa, Nick Reynald aliyezaliwa Zimbabwe na kuishi Tanzania kwa miaka 18 yaani
tangia mwaka 1998 atakuwa balozi mzuri kwa uitalii wa Tanzania kwa sababu
maeneo mengi ya utalii anayajua.
“Nick Reynald
‘Bongozozo’ ameishi hapa nchini kwa miaka mingi kuanzia mwaka 1998 mpaka sasa
ni miaka 18 kwa hiyo anauelewa na utalii wa Tanzania, amekuwa maarufu sana hapa
nchini kutokana na mapenzi makubwa kwa
Tanzania ambayo yemejidhihirisha katika nyanja nyingi ikiwemo ushabiki wa mpira
kwa timu ya Taifa ‘Taifa Stars” pamoja na wachezaji akiwemo Mbwana Samatta
anayekipiga kunako klabu ya mpira ya Astoni villa nchini Uingireza”, Alisema
Geofrey Meena.
0 comments:
Post a Comment