Kaimu Mkuu
wa Kanda ya Kati wa Shirika la Viwango Tanzania, Bi. Salome Emmanuel, akiwaonesha
waandishi wa habari bidhaa zisizokidhi viwango na kuisha muda wake wa
matumizi wakati wa zoezi la uteketezaji
wa bidhaa hizo lililofanyika leo Januari 16, 2020 katika dampo la Chidaya Jijini Dodoma.
Sehemu ya
bidhaa zilizokamatwa kwenye zoezi la kubaini bidhaa zilizoisha muda wa matumizi zikiwa
tayari kuteketezwa leo Januari 16, 2020 katika Dampo la Chidaya Jijini Dodoma.
Oparesheni hiyo imefanikiwa kukamata bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni kumi.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza
bidhaa zenye thamani ya shilingi milioni 10 kwa kukosa kukidhi ubora.
Akizungumza wakati wa zoezi la uteketezaji wa
bidhaa hizo zikiwemo vipodozi, vyakula na vinywaji, Kaimu Mkuu wa Kanda ya Kati
ya Shirika hilo Bi. Salome Emmanuel amesema kuwa baadhi ya bidhaa
zilizoteketezwa ni zile ambazo muda wake wa matumizi umekwisha na bado
wafanyabiashara wasio waadilifu walikuwa wakiendelea kuziuza.
“Ukaguzi tuliofanya kati ya mwezi Oktoba na
Desemba 2019 katika mikoa ya Dodoma na Singida umetuwezesha kubaini bidhaa hizi
ambazo baadhi ya bidhaa zizisokidhi viwango na nyingine muda wake wa matumizi
umekwisha lakini bado wafanyabiashara
wasio waaminifu wamekuwa wakiendelea kuziuza” alisisitiza Bi. Solome
Akifafanua Bi. Solome amesema kuwa Shirika
hilo litaendelea kufanya ukaguzi mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa bidhaa
zilizopo sokoni zinakidhi vigezo kwa mujibu wa sheria.
Aliongeza kuwa wananchi wana jukumu la
kushirikiana na shirika hilo katika kuhakikisha kuwa wafanyabiashara wasio
waadilifu hawafanikiwi kuuza bidhaa ambazo muda wake umekwisha na ambazo
hazikidhi vigezo.
Aidha, aliwataka wafanyabiashara wote
kuzingatia sheria na kanuni pale wanapotaka kuingiza bidhaa hapa nchini na hata
wale wanaofanya uzalishaji hapa nchini.
Kwa upande wake mkaguzi wa Chakula wa Shirika
hilo Bw. Abel Deule amesema kuwa Shirika
hilo linaendelea kuhakikisha kuwa wananchi wanalindwa dhidi ya bidhaa zisizo na
ubora na zile ambazo muda wake wa matumizi.
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limekuwa
likifanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakikisha kuwa bidhaa zinazoingia
nchini zinakidhi vigezo .
0 comments:
Post a Comment