Na Mwandishi Wetu Tukuyu Mbeya
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akitazama
sampuli zilizopo katika Ofisi ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu
NIRM Tawi la Tukuyu wakati wa ziara yake kutembelea na kujionea utendaji kazi
wa Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akiwa
katika picha ya pamoja na watumishi wa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu na Kanda ya Mbeya wakati wa ziara yake kutembelea
na kujionea utendaji kazi wa Taasisi hiyo.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile ameshuhudia Ofisi
ya Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu
ilivyotelekezwa na kutojishughulisha na tafiti zozote ndaniya kipindi cha muda
mrefu.
Dkt. Ndugulile amebaini hayo Tukuyu
mkoani Mbeya wakati wa ziara yake katika Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya
Binadamu NIRM Tawi la Tukuyu kujionea utendaji wa Taasisi hiyo.
Dkt. Ndugulile ameitaka Taasisi ya
Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM kurudisha Tawi la Tukuyu katika hali yake
ya awali kama ilivyokuwa ikisifika miaka ya nyuma ikiwa imejikita katika
taifiti.
Naibu Waziri Dkt. Ndugulile ameitaka
Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu NIRM kufanya tafiti zaidi bila ya
kutegemea sana wadau kwani zipo fedha za ndani zilizotengwa na Serikali kwa
ajili ya kufanya tafiti zikiwemo tafiti za magonjwa ya binadamu.
Ameongeza kuwa kumekuwa na matatizo
mengi ambayo yamekuwa yakiwakabili wananchi ikiwemo kutumia dawa bila kuwa na
malaria, UTI na Typhoid ikiwa ni asilimia 70 ya homa zikihusishwa na
magonjwa hayo hivyo Taasisi hiyo ina nafasi kubwa ya kufanya utafiti katika
hili na kuwapa majibu wananchi.
“Nimesikitishwa sana na utendaji
kazi wa kituo hiki cha Tukuyu na wote naona mmehamia Mbeya nataka nione
mabadiliko katika Taasisi hiii hasa kituo hiki cha Tukuyu” alisema Dkt.
Ndugulile
Dkt. Ndugulile amemtaka Mkurugenzi
wa NIRM kusema kama hawana matumizi ya ofisi ya Tukuyu ili itumike kwa matumizi
mengine kwani haoni kinachofanyika katika Taasisi hiyo nyeti katika tafiti za
magonjwa ya binadamu nchini iliyopo Wilayani Rungwe.
“Tunataka kukiona hiki kituo kirudi
katika heshima yake iliyokuwa nayo siku za nyuma hapa kusiwe ni sehemu ya
mapumziko ya watumishi bali kitumike kufanya tafiti”
alisema Dkt. Ndugulile
Kwa upande wake Mkurugenzi NIRM
Mbeya Dkt. Nyanda Elias Ntinginya amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa bado
wanahiitaji Ofisi ya NIRM Tukuyu kwani bado kuna tafiti zinahitajika ili
kuwasaidia wananchi.
Ameongeza kuwa Taasisi hiyo
itawakilisha mpango mkakati wa kuiendehsa Ofisi ya Tukuyu ndani ya mwezi mmoja ili
kuhakikisha Taasisi hiyoiatekelza majukumu yake ipasavyo katika kuhakikisha
inawasaidia kujibu maswali ya wananchi kuhusu magonjwa ya binadamu.
0 comments:
Post a Comment