Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(
katikati) akiwasili katika Wilaya ya Handeni Mkoani Tanga kwa ziara ya kikazi
ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini, Mei 9,2020, wa pili kushoto
ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Godwin Gondwe.
Baadhi ya Watendaji wa wilaya ya Handeni,
Wakandarasi wanaotekeleza mradi wa usambaji wa umeme vijijini wilayani humo
pamoja na baadhi ya watendaji wa Wizara ya
Nishati na Taasisi zilizochini yake,wakimsikiliza Waziri wa Nishati,
Dkt. Medard Kalemani kabla ya kuanza ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji
umeme vijijini katika wilaya hiyo, Mei 9,2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani
(kushoto) akizungumza na mmoja wa mwenye nyumba katika kijiji cha Kwasunga
wilayani Korogwe Mkoani Tanga, baada ya kuwasha umeme katika nyumba
hiyo,alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya usambazaji umeme vijijini katika
wilaya hiyo Mei 9, 2020.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani(
kulia),Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe, Rahel Muhando(kushoto) kwa niaba ya
Mkuu wa Wilaya hiyo, wakikagua kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kilole
wilayani Korogwe, Mei 9,2020, kituo hicho kilijengwa 1929 kwa sasa kinafanyiwa
ukarabati kuboresha utendaji kazi wake.
Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani(
kushoto)akitoa maelekezo kwa msimamizi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme
cha Kilole,wilayani Korogwe mkoani Tanga, Mhandisi Peter Magari, wakati waziri
wa Nishati alipofanya ziara ya kushtukiza kutembelea kituo hicho kilichojengwa
1929 ambacho kinafanyiwa ukarabati kubosha utendaji kazi wake.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema
mkandarasi yeyote aliyepewa jukumu la kutekeleza mradi ya REA akishindwa
kukamilisha kazi hiyo ifikapo Juni 31, 2020 kama ilivyoelekezwa katika
makubaliano ya mkataba atakatwa asilimia kumi(10%) ya yalipo yake yaliyosalia.
Dkt. Kalemani alitoa kauli hiyo wakati akifanya
ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa usambazji wa
umeme vijijini katika Wilaya za Handeni, Korogwe na Lushoto Mkoani Tanga, Mei
09, 2020.
Alisema kuwa kwa mujibu wa mkataba, wakandarasi
wote nchini waliopewa kazi ya kutekeleza mradi wa usambazaji umeme vijijini
wanatakiwa kukamilisha kazi hiyo ifikapo mwezi Juni 30,2020, kwa wilaya za
mikoa yote nchini, na atakayeshindwa kufanya hivyo mradi huo utakabidhiwa kwa
mkandarasi mwingine na atakatwa asilimia
kumi ( 10%) ya malipo yaliosalia.
Dkt. Kalemani alisisitiza kuwa endapo, mkandarasi
atatakwa asilimia kumi (10%) ya malipo yake yaliyosalia,fedha hizo zitapelekwa
kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha,( HAZINA) ili zitumike kumlipa mkandarasi
mwingine atakayepewa jukumu la kukamilisha mradi huo.
“Hakuna sababu ya msingi ya kumfanya mkandarasi
ashindwe kukamilisha mradi huo kwa mujibu mwa mkataba, pia itanishangaza
akishindwa kufanya hivyo kwa sababu fedha zote za awali walishalipwa na vifaa
vyote vipo na vinapatikana hapa nchini, tunataka kukamilisha kazi hii ndani ya
wakati ili tusonge mbele, kwa hili sitamvumilia yeyote”, alisema Dkt. Kalemani.
Katika ziara hiyo Dkt. Kalemani aliwasha umeme
katika Kijiji cha Kisasu Kata ya Sindeni wilayani Handeni, pia katika kijiji
cha Kwasunga wilayani Korogwe, na katika kijiji cha Kwamsale Kata ya Emtoye
wilayani Lushoto mkoani Tanga.
Aidha aliwaagiza Viongozi wa Serikali za Mitaa
waliofika katika shughuli za uwashaji umeme kwa niaba ya wananchi wao,ili
kuepuka mikusanyiko isiyo ya lazima ikiwa ni tahadhari ya kujikinga na maambuki
ya Corona, kuwahimiza na kuwasisitiza wananchi wao kuendelea kulipia gharama za
kuunganishwa umeme ya shilingi 27,000 tu .
Pia wasikubali kulipia miundombinu ya umeme
kama, nguzo, nyaya, mita za luku na mashineumba kwakuwa tayari zimekwisha
lipiwa na serikali.
Katika ziara hiyo pia alitembelea Kituo cha
Kupoza na Kusambaza umeme cha Kilole kilichopo wilayani Korogwe mkoani Tanga,
kilichojengwa mwaka 1929 chenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2.5 ambacho kwa
sasa kinafanyiwa ukarabati mkubwa.
Dkt. Kalemani aliuagiza uongozi wa Shirika la
Umeme Nchini( TANESCO) kukamilisha ukarabati huo ifikapo June 15, 2020, mwaka
huu ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa umeme kwa wakazi wa Walaya ya
Korogwe mkoani humo.
Vilevile aliuagiza TANESCO kutafuta eneo kubwa
zaidi ili kukihamisha kituo hicho ambacho kiko katika eneo finyu na
kimezingirwa na makazi ya watu.
Alisema kuwa endapo kituo hicho kitahamishiwa
katika eneo kubwa zaidi kitakuwa na fursa ya kuongezewa uwezo zaidi na hata
kujengwa mitambo mingine mikubwa ya kupoza na kusambaza umeme kwa watumizi
mengine hapo baadaye.
Ukarabati unaofanyika katika kituo hicho ni
kufunga mashineumba mpya yenye uwezo wa kuzalisha Megawati tano za umeme,
kuweka vifaa na miundombinu mipya ya kituo hicho pamoja na kutenganisha njia za
kusafirisha umeme kutoka katika kituo hicho kwenda kwa watumiaji.
“Mnasubiri nini kufunga hii mashineumba ambayo
imefika hapa miezi miwili iliyopita?,pia harakisheni ukarabati kwa kubadilisha
miundombinu ya kituo hichi, iliyopo hapa ni chakavu si mnaiona na niyazamani
sana jamani,wananchi watanga wanataka umeme mwingi na wa uhakika, na marufuku
kukatika umeme kwa mkoa huu mara baada ya kukamilika kazi hii”, alisisitiza
Dkt. Kalemani.
Kuhusu suala la wizi wa umeme na miundombinu
yake, Dkt. Kalemani alisema kuwa yeyote atayebainika kufanya vitendo vya wizi
ni muhujumu uchumi hivyo achukuliwe hatua za kisheria.
Aliwataka wananchi kwa kushirikiana na mamlaka
husika kulinda miundombinu ya umeme pia kuwaweka bayana na kuwataja wale wote
wenye tabia ya wizi ili wachukuliwe hatua, kuepuka kuleta usumbufu kwa wananchi
kwa kukosa huduma ya umeme na hasara kwa serikali.
Sambamba na hilo aliwataka watumishi wa TANESCO
kuwa na weledi na wazalendo wakati wa kutekeleza majukumu yao kwa kuwa baadhi
yao huchafua sifa za shirika hilo kwa kijihusisha na vitendo vya wizi kwa
kushirikiana na watu walionje ya shirika hilo.
Kwa upande wao wakuu wa wilaya za mkoa huo,
akiwepo Mkuu wa wilaya ya Handeni Godwin Gondwe, Katibu Tawala, Rahel Muhando
kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe na Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Januari
Lugangika, walimuahidi Dkt. Kalemani kuyafanyia kazi na kutekeleza maagizo
aliyoyatoa, kwa lengo la kuhakisha wananchi wote wanapata umeme utakaochochea
shughuli za kiuchumi na maendeleo kwa jumla.
0 comments:
Post a Comment