Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ghala la kuhifadhia mbolea la Stamco katika eneo la Vwawa wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019. (Picha Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya Umwagiliaji ya Mbulu iliyopo katika kata ya Mahenje wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua ghala la kuhifadhia mbolea la Stamco katika eneo la Vwawa wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akikagua skimu ya Umwagiliaji ya Mbulu iliyopo katika kata ya Mahenje wilayani Mbozi wakati akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe tarehe 22 Disemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo-Songwe
Serikali
imeeleza kuwa imekusudia kuanzisha juhudi wezeshi kuhakikisha kuwa mbegu bora
za kilimo zinazalishwa nchini ili kuondokana na wimbi la uagizaji wa mbegu nje
ya nchi.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameyasema hayo tarehe 22 Disemba 2019 mara
baada ya kutembelea kampuni ya Namburi inayojihusisha na uzalishaji wa mbegu za
vizazi za mahindi, mtama na mpunga iliyopo katika eneo la Vwawa wilayani Mbozi wakati
akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Songwe.
Amesema
kuwa Tanzania ina uhitaji wa mbegu kiasi cha Tani 186,000 za mazao mbalimbali
huku uzalishaji wa ndani ikiwa ni pamoja na uagizaji wa mbegu nje ya nchi ukiwa
bado mdogo kwani haujafika hata Tani 50,000.
Amesema
kuwa Tanzania ina maeneo makubwa na bora kwa uzalishaji hivyo ni lazima
kuzalisha mbegu za kutosha nchini na kuachana na utegemezi wa mbegu kutoka nje
ya nchi.
Waziri
Hasunga ametoa rai kwa wananchi kuhakikisha kuwa wananunua mbegu bora kwa ajili
ya kukabiliana na msimu wa kilimo na kuachana na matumizi ya mazao yao ya
misimu iliyopita waliyoyahifadhi kama mbegu.
Katika
ziara hiyo waziri Hasunga amezungumza na wananchi wa kijiji cha Mbulu kilichopo
katika kata ya Mahenje wilayani Mbozi mara baada ya kukagua skimu ya
umwagiliaji ya Mbulu amesema kuwa serikali imedhamiria kuimarisha skimu za
umwagiliaji nchini ili kuondokana na kilimo cha kutegemea mvua.
Mhe
Hasunga amesema kuwa kilimo cha kutegemea mvua ni hatari kwani hakina uhakika
wa upatikanaji wa chakula cha kutosha kutokana na changamoto mbalimbali
zinazojitokeza za kukosekana kwa mvua kwa sababu ya mabadiliko ya tabia nchi.
Amewaagiza
maafisa ugani kuzuru katika maeneo ya wakulima ili kutoa elimu sahihi za
kilimo, matumizi sahihi ya viuatilifu pamoja na matumizi sahihi ya zana za
kilimo.
Ameitaja
Programu ya kuendeleza kilimo awamu ya pili-ASDP II yenye jukumu la kuimarisha
masoko na kuongeza thamani kuwa ni lazima wakulima watumia njia bora za kilimo
ikiwa ni pamoja na kupata elimu bora na sahihi kwa wakulima.
Waziri
Hasunga amesema kuwa katika Programu hiyo ya kuendeleza kilimo awamu ya pili
moja ya mambo msingi ni matumizi bora ya maji na ardhi, hivyo sekta ya kilimo
ni muhimili wa matumizi bora ya maji kupitia skimu za umwagiliaji.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment