KAMANDA wa polisi mkoani Pwani,
Boniventure Mushongi, akionyesha vifaa vilivyotumika katika matukio
mbalimbali ya kiuhalifu mkoani hapo, ikiwemo shortgun, bastola, risasi,
visu na vingine. (picha zote na Mwamvua Mwinyi).
Na Mwamvua Mwinyi, Pwani
JESHI la polisi Mkoani Pwani
linawashikilia watu 20 kwa kosa la kuhusika na uuzaji wa dawa
mbalimbali za kulevya ikiwemo heroin,mirungi na bangi .
Aidha limekamata nyara za serikali ,meno ya tembo sita thamani yake mil.98.100 na vipande 56 vya ngozi ya mbalawa .
Jeshi hilo pia limefanikiwa
kukamata magunia ya bangi 28, puli 270 ,heroin kete 700 ,lita 522 za
pombe ya moshi (gongo) na mitambo saba ya kutengeneza pombe
hiyo,misokoto 52 ,kete 2,853 na mirungi milaa 94 .
Akizungumzia juu ya matukio
hayo ,kamanda wa polisi mkoani Pwani, Boniventure Mushongi alisema, pia
wamewakamata wahamiaji haramu 153 ambapo kati ya hao saba walikutwa
wakisafirishwa kwenye gari namba T.568 CZG .
Alieleza ,kuna mazao ya misitu
yasiyokuwa na vibali nayo yamekamatwa ikiwa ni pamoja na mkaa magunia
71 na ambao 117 ,sukari viroba 23 vya kg hamsini na mchele viroba 12 vya
kg 12 ,simu za mkononi 29 na nondo tani 10.
Hata hivyo ,kamanda Mushongi,
alisema mafanikio hayo yametokana na operesheni iliyofanyika ndani ya
wiki mbili baada ya kutokea tukio la mauaji ya aliyekuwa mkuu wa wilaya
ya Liwale Ephraim Mfingi Mbaga (54).
“Katika operesheni hiyo
wamekamatwa watu 15 ambao wamekiri kujihusisha na matukio ya uporaji na
mauaji kwenye matukio mbalimbali mkoani hapo”
“Kadhalika wahalifu hao
walikiri kujihusisha na matukio ya uvamizi na kusababisha vifo kwa
Zawadi Dephara na Edward Chamuhene wote wawili wakiwa ni wakazi wa
Misugusugu na Mtengi Mabuga mkazi wa Boko ” alisema.
Kamanda Mushongi, alifafanua
kuwa bastola mack IV moja yenye namba 1944 na risasi zake tatu ,bastola
moja yenye namba A.1944 na risasi zake nne, short gun mbili nazo
zimekamatwa.
Alisema walifanikiwa kuipata
baada ya kutelekeza kwenye tukio la ujambazi kufuatia aliyekuwa
akiimiliki silaha hiyo kujeruhiwa wakati wa tukio hilo huko maeneo ya
Misufini ,Mlandizi .
“Ikiwa imekatwa mtutu model
305 KB 12 na shortgun ya pili yenye namba 30102 pamoja na silaha aina ya
gobole moja na risasi zake 19.
Kamanda Mushongi ,alibainisha
,tangu jan 2017 hadi sasa wamefanya operesheni katika maeneo mbalimbali
ya mkoa na kukamata watuhumiwa 579 walifanya makosa mbalimbali .
Alisema wanaendelea na operesheni hiyo ambayo imeanza na wamejipanga kukabiliana na uhalifu wa aina yoyote.
0 comments:
Post a Comment