METDO Tanzania

METDO Tanzania

Tuesday, December 24, 2019

DKT TULIA AZINDUA MASHINA MATATU YA CCM MKOANI MBEYA


Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson amefanya ziara katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mbeya ambapo pia amezidua jumla ya mashina matatu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiwemo shina la wakereketwa Hasanga, Shina la Makasini stendi pamoja na Stendi mpya.
Pamoja na hayo Dkt. Tulia kupitia taasisi yake ya Tulia Trust ametoa msaada wa jezi za mpira kwa wanavikundi, bima za afya kwa wazee wasiojiweza ambao ni wanachama wa mashina hayo.
Zaidi ya hapo Dkt. Tulia amewataka wananchi kupuuza kauli za baadhi ya viongozi wakiwemo wa vyama vya upinzani wanaowataka kutowatambua na kushirikiana na wenyeviti wa Serikali za mitaa kwa kile wanachodai uchaguzi haukuwa huru na haki.
Dkt. Tulia amesema>>>“Niwaombe sana ndugu zangu tuendelee na ushirikiano wa kujenga taifa letu, usikatae kushirikiana na kiongozi ambaye upo naye. Waswahili tunasema fimbo ya mbali haiui nyoka, sasa wewe unamsikiliza mtu yupo Dar es salaam anatoa tamko na wakati huohuo yeye mwenyewe anashirikiana na viongozi wakuu alafu anakudanganya wewe usishirikikiane na viongozi wako”
“Tushirikiane na viongozi tuliowachagua, na tunasema tumewachagua kwasababu ukiwa uwanjani ukipigwa kwa penati au dakika tisini hata kama ni dakika za nyongeza kote ni kupigwa tu na wakubali yakuwa wamepigwa”-Dkt. Tulia
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com