METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, December 20, 2019

SERIKALI YATAJA SEKTA ZINAZOONGOZA KWA MIGOGORO YA KAZI NCHINI



Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama amezitaja taasisi zinazoogoza kwa kuwa na migogoro ya kikazi nchini hali ambapo husababisha kutumika vibaya kwa rasilimali muda kati ya mwajiri na Mfanyakazi hali inayopelekea kuchelewesha Maendeleo.    

Waziri Mhagama ameyasema hayo leo, tarehe 19, Desemba 2019,  mjini Morogoro,  wakati akifungua kikao kazi cha Tathmini ya utekelezaji wa Majukumu ya Tume kilichowakutanisha Wasuluhishi na  Waamuzi wa migogoro ya kikazi na wasaidizi wa Tume hiyo. Aidha, amefafanua kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu Kupitia Tume hiyo  imepewa jukumu la kutatua migogoro na kuweka msisitizo wa kuimaliza migogoro.

Aidha, Mhe. Mhagama ameitaka Tume hiyo kuendelea kufanya utafiti kwa sekta   zote zinazoongoza kwa migogoro ya kikazi ili kubaini chanzo cha migogoro hiyo na kuandaa Mkakati Maalum wa kuishughulikia, ili kuhakikisha migogoro ya kikazi haizalishwi mahala pa kazi.

Tume ya Usuluhishi na Uamuzi  ipo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu, ambapo  Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Tume hiyo kimefanyika kwa mujibu wa Agizo la Rais Na.1 la mwaka 1970. Baraza hilo   huiwezesha Tume kuboresha Huduma na masuala ya utatuzi Wa migogoro ya kikazi kwa njia ya Usuluhishi na Uamuzi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com