Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Mbunge wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga akisisitiza jambo kuhusu upatikanaji wa umeme katika jimbo la Vwawa wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Baadhi ya wananchi wa Jimbo la Vwawa Mkoani Songwe wakifatilia mkutano wa Mbunge wa jimbo hilo ambaye ni Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga wakati akiwa katika ziara ya kikazi jimboni kwa ajili ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi.
Na Mathias Canal, Songwe
Serikali imesema hakuna
kijiji nchini kitakachoachwa bila ya kuunganishiwa umeme katika awamu ya tatu
ya mradi unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (Rea).
Aidha, Serikali imetenga Trilioni 1 kwa ajili ya
kusambaza umeme katika vijiji 8,000 ambavyo bado havijaunganishiwa na nishati
hiyo huku ikiendela na uwekaji wa umeme katika vijiji vingine zaidi ya 13400 kote nchini.
Mbunge wa Jimbo la
Vwawa Mkoani Songwe Mhe Japhet Hasunga amewahakikishia wananchi kuhusu
upatikanaji wa umeme katika jimbo hilo hivyo wananchi wanapaswa kuondoa
wasiwasi na serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli.
Mhe Hasunga ameyasema hayo wakati
wa mikutano yake katika kijiji cha Igale na Iyula A vilivyopo katika kata ya
Iyula akiwa katika ziara ya kikazi jimboni humo iliyoanza juzi tarehe 22 Disemba 2018.
Alisema kuwa upatikanaji wa umeme
katika jimbo lake utasaidia kuongeza upatikanaji wa huduma mbalimbali za
kijamii na kuwa chachu ya maendeleo kwa wananchi na Taifa kwa ujumla wake.
Alisema kuwa utekelezaji wa
Miradi hiyo ya umeme katika Jimbo la Vwawa unaenda sambamba na lengo la
Serikali ya awamu ya Tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda ifikapo
2025.
Mhe Hasunga amewataka
wananchi hao kutumia fursa mbalimbali zitakazotokana na utekelezaji wa miradi
katika sekta ya gesi na mafuta ili kujiongezea kipato na kuiwezesha nchi
kutimiza malengo yake kuelekea kuwa nchi ya uchumi wa kati.
Kuhusu
malalamiko ya wananchi dhidi ya gharama kubwa za pembejeo za kilimo, Mhe
Hasunga ambaye ni Waziri wa Kilimo amewahakikishia wananchi kuwa wizara yake
imejipanga kuhakikisha kuwa mbolea zinapatikana kwa wakati ili wakulima wa
mazao mbalimbali ya chakula na biashara waweze kunufaika na pembejeo hizo.
Alisema
kuwa kumekuwa na malalamiko mengi nay a muda mrefu kuhusu mbolea hivyo serikali
itapitia upya utaratibu wa uuzaji wa mbolea ili kutafuta namna bora ya
kurahisisha huduma hiyo kwa wakulima nchini.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment