Mkuu wa
Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amechangia shilingi milioni tatu ili
kuharakisha ukarabati wa ujenzi wa shule ya msingi Msia pamoja na shule ya
sekondari Kipeta zote za bonde la ziwa rukwa, Wilayani Sumbawanga ikiwa ni
kuunga mkono juhudi za wananchi katika kurudisha miundombinu ya shule hizo
zilizoharibika baada ya upepo na mvua kali iliyonyehs amwanzoni mwa mwezi huu.
Kati ya
fedha hizo shilingi milioni mbili zitatumika katika shule ya msingi Msia na
shilingi milioni moja zitatumika kuikarabati shule ya sekondari kipeta ambapo
zimebaki wiki mbili shule hizo kufunguliwa na wanafunzi kutakiwa kuendelea na
masomo.
Mh.
Wangabo aliwashukuru wananchi waliojitokeza kuchangisha fedha kwaajili ya
ukarabati wa shule ya msingi Msia zilizofikia kiasi cha shilingi 5,595,000/=
ambapo wananchi wa kawaida walichangia shilingi 5000/=, wafanyabiashara wadogo
shilingi 20000/=, mfangabiashara wa kati shilingi 50000/= na wafugaji shilingi
100000/= ambapo fedha hizo zinatarajiwa kufanya ukarabati na ujenzi wa madarasa
manane.
Awali
akisoma taarifa ya harambee ya ukarabati wa shule Mtendaji wa kijiji cha Msia
Andrew Sanga alieleza mikakati ya kijiji kuwa ni kuongeza vyumba vya madarasa
vitatu, na ofisi moja ya walimu na msingi umeshaaza kujengwa, kukusanya
michango kwa wananchi ambao bado kuchangia na hivyo kutimiza lengo la kujenga
madarasa nane, ofisi mbili ndani kabla ya shule kufunguliwa mwanzoni mwa mwezi
wa kwanza.
“Mheshimiwa
mkuu wa mkoa mapungufu yaliyopo ni kama ifuatavyo, bati, madirisha, nondo,
misumari, madirisha, milango na rangi, ili kukamilisha majengo tunayoendelea
kuyajenga kwani shule hiyo yenye wanafunzi 866 ina uhitaji wa madarasa 22,”
Alibainisha.
Katika
kuunga Mkono juhudi hizo Mh. Wangabo alisema,”Pamoja na pongezi ambazo
nilizitoa kwa wadau wote ambao wamechangia, na mimi nipende kushirikiana nanyi,
nitachangia vifaa ambavyo inaweza ikawa mabati, au inaweza ikawa saruji,
kulingana na hesabu zitakazokuwa zinapigwa na Mkurugenzi pale, nitachangia
hivyo vifaa kwa shilingi milioni mbili.”
Pia
aliwasihi mafundi wa madarasa hayo kujiahidi kuzingatia ubora katika ujenzi
kuliko ilivyokuwa imejengwa hapo awali na kuwaomba wachukulie kazi hiyo ni kama
ya kujitolea mchango wao katika kuunga juhudi za wananchi kumaliza shule hiyo.
Pia kwa
upande wa shule ya sekondari ya Kipeta alichangia shilingi milioni moja kama
mwanzo wa harambee itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa kwanza mwaka 2019 ili
kuhamasisha wananchi wa kijiji cha kipeta kuweza kuiboresha shule hiyo ambayo
iliezuliwa mapaa yote pamoja na baadhi ya nyumba 4 za walimu ikiwemo ya mwalimu
Mkuu.
Kwa
upande wake Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Sebastina
Mwilima alisema kuwa tayari halmashauri imeshaagiza vifaa vyenya thamani ya
shilingi milioni 23 kwaajili ya kufanikisha zoezi la kukarabati shule hizo
ambapo shule ya msingi Msia madarasa manne yalianguka na shule ya sekondari
Kipeta, madarasa, mabweni pamoja na nyumba za waalimu kuezuliwa mapaa.
Maelezo
ya Picha
IMG_5456
- Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa pili toka kulia) pamoja na Mkuu
wa Wilauya ya Sumbawanga Dkt. Khalfan Haule (wa kwanza Kulia) wakipita mbele ya
madarasa ya Shule ya Msingi Msia kuona uharibifu uliofanywa na mvua ya tarehe
8.12.2018.
IMG_5462
- Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa kwanza kushoto)akionyeshwa
maendeleo ya ujenzi wa madarasa unaoendelea ili kuhakikisha shule
inapofunguliwa mwezi wa kwanza wanafunzi wanapata fursa ya kuendelea na
masomo.
IMG_5474
- Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akishiriki msingi wa ujenzi wa
madarasa ya shule ya msingi Msia alipokwenda kuangalia ujenzi
unaoendelea.
IMG_5496 - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim
Wangabo.
Kipeta
Sekondari - Jengo la Utawala la shule ya Sekondari Kipeta likiwa limeezuliwa
paa.
0 comments:
Post a Comment