Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (katikati) alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika mkoa wa Arusha akiambatana Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo (kushoto)
Waziri wa Viwanda na Biashara Innosent Bashungwa pamoja
na Mhe Gambo wamekitembelea kiwanda cha HANSPAUL AUTOMECHS LTD Kinachohusika na
utengenzezaji na uboreshaji wa Magari ya kitalii
Waziri wa Viwanda
na Biashara Innocent Bashungwa akiwa Mkoani
Arisha pia ametembelea kiwanda cha HANSPAUL INDUSTRIES LTD kinachojihusisha na
utengenezaji wa Karatasi na Vifungashio.
Baada ya kutemelea viwanda hivyo Waziri Bashungwa
amepongeza wawekezaji kwa kuona fursa na kuamua kufanya uwekezaji katika viwanda
kwenye Mkoa wa Arusha, Pia amewaahidi kutatua changamoto wanazozipata kwa muda mfupi huku akiwaunganisha
na kiwanda cha utengenezaji wa magari cha GB Auto Group kilichopo Kairo Misri
alichokitembelea wiki iliyopita.
0 comments:
Post a Comment