Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akitoa heshima za mwisho kwa mama mzazi wa Naibu wake Dkt Angeline Mabula aliyefiwa na mama yake mzazi Bi Cecilia Lubala wakati wa kuaga mwili wa marehemu eneo la Ishungisha wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa kwanza kulia) pamoja na ndugu zake wakiweka shada la maua katika kaburi la mama yake mzazi bi Cecilia Lubala baada ya kukamilika kwa mazishi katika kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza jana.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula (wa pili kushoto) wakati wa mazishi ya mama yake mzazi Bi Cecilia Lubala baada ya kukamilika kwa mazishi katika kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza jana. Wa tatu kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania Qween Mlozi.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akiwa na viongozi wengine katika mazishi ya mama mzazi wa Naibu wake Dkt Angeline Mabula Bi Cecilia Lubala katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Mnyengeja wilayani Kwimba mkoa wa Mwanza jana.
…………………
Na Munir Shemweta, WANMM MWANZA
Mamia ya wananchi wa jiji la Mwanza na vitngoji vyake wamejitokeza kwa wingi kumzika mama mzazi wa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula.
Mazishi ya Mama Mzazi wa Dkt Mabula Bi Cecilia Lubala yamefanyika jana kwenye makaburi ya familia yaliyopo kijiji cha Mnyengeja kata ya Sumve wilaya ya Kwimba mkoani Mwanza.
Kabla ya mazishi hayo yaliyohudhuriwa pia na viongozi wa Chama na Serikali kulifanyika ibada maalum ya kumuombea marehemu Cecilia Lubala kwenye Kanika Katoliki Parokia ya Kirumba na baadaye shughuli ya kuaga mwili eneo la Ishungisha wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza.
Miongoni mwa viongozi waliohudhuria mazishi hayo ni Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo William Lukuvi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Kilagi, Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Herry Jemes, Katibu wa UWT Queen Mlozi, Mkuu wa mkoa wa Katavi Anthony Mtaka, Wakuu wa wilaya na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Marehemu Cecilia Lubala alifariki dunia jumamosi iliyopita tarehe 23 Novemba 2019 baada ya kuugua kwa muda mrefu na kulazwa kwa nyakati tofauti katika hospitali za Muhimbili, Dodoma na Bugando mkoani Mwanza ambako umaiti ulimkuta.
0 comments:
Post a Comment