Friday, November 29, 2019

ZIARA YA WAZIRI BASHUNGWA MKOANI ARUSHA, ATEMBELEA VIWANDA NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Innocent Bashungwa (katikati) alipokuwa kwenye ziara ya kikazi katika mkoa wa Arusha akiambatana Mkuu wa Mkoa Arusha Mrisho Gambo (kushoto)

Waziri wa Viwanda na Biashara Innosent Bashungwa pamoja na Mhe Gambo wamekitembelea kiwanda cha HANSPAUL AUTOMECHS LTD Kinachohusika na utengenzezaji na uboreshaji wa Magari ya kitalii

Waziri  wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa  akiwa Mkoani Arisha pia ametembelea kiwanda cha HANSPAUL INDUSTRIES LTD kinachojihusisha na utengenezaji wa Karatasi na Vifungashio. 
Baada ya kutemelea viwanda hivyo Waziri Bashungwa amepongeza wawekezaji kwa kuona fursa na kuamua kufanya uwekezaji katika viwanda kwenye Mkoa wa Arusha, Pia amewaahidi kutatua changamoto  wanazozipata kwa muda mfupi huku akiwaunganisha na kiwanda cha utengenezaji wa magari cha GB Auto Group kilichopo Kairo Misri alichokitembelea wiki iliyopita.

No comments:

Post a Comment