Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dodoma wakati
akizungumzia kuelekea kwenye upingaji kura Uchaguzi Serikali za Mitaa
utakaofanyika kesho nchini kote.
Baadhi ya waandishi wa
habari kutoka vyombo vya habari mbalimbali wakimsikiliza Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,wakati
akizungumzia upingaji kura Uchaguzi Serikali za Mitaa utakaofanyika
kesho nchini kote.
…………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Kuelekea katika uchaguzi
wa serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika hapo kesho, Waziri wa Nchi
Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo,
amewataka wananchi kushiriki katika zoezi hilo bila kujihusha na
viashiria vya uvunjifu wa amani au kuvuruga uchaguzi huo.
Pia amesema uchaguzi huo
utafanyika katika maeneo mbalimbali hapa nchini isipokuwa mikoa mitatu
ya Katavi, Ruvuma na Tanga ambapo wagombea wake katika vyama mbalimbali
walipita bila kupingwa.
Waziri Jafo ameyasema
hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na wanahabari kuhusu uchaguzi
huo unaotarajiwa kufanyika kesho maeneo mbalimbali hapa nchini, Waziri
Jafo amewataka wananchi na wagombea kutojihusisha na vitendo vyovyote
vitakavyopelekea kuharibu uchaguzi huo.
” Niwaombe wa Tanzania
kwa umoja wao wahakikishe zoezi hilo linafanyika kwa amani na utulivu na
kuchagua viongozi watakaowafaa katika maeneo yao, wajiepushe na vitendo
vya kupiga Kampeni wakati wa kupiga kula, na ikiwamo kuvaa sare za
vyama vyao” amesema Waziri Jafo.
Huku akibainisha kuwa
zoezi la uchaguzi litafanyika katika maeneo mbalimbali isipokuwa katika
mikoa ya Tanga, Ruvuma na Katavi ambako wagombea wao katika vyama
mbalimbali walipita bila kupingwa hivyo zoezi hilo halitawahusu.
Ameongeza kuwa ”
zoezi la kupiga kura litaanza saa mbili kamili asubuhi na kumalizika saa
kumi kamili jioni na wale wote ambao muda huo utawakuta kwenye foleni
wataruhusiwa kupiga kura wakati wale watakaofika baada ya mda huo
hawataruhusiwa kupiga kura kabisa” amesema.
Aidha amesisitiza
wale wenye mahitaji maalumu kupewa kipaumbele kama vile walemavu, Wazee,
wajawazito na wenye watoto wadogo kama desturi ya watanzania waliyozoea
siku zote.
Amesema vyama vyote
vitakuwa na mawakala ambao watasimamia mazoezi hayo yote kuanzia kupiga
kura hadi zoezi la kuhesabu kura ili kila mtu apate haki yake ya
kimsingi katika uchaguzi huo, na watahakikisha matokeo ya maeneo yote
yatapatikana kesho hiyohiyo.
Amesema vyama vyote
kumi na tisa(19)vyenye usajili itashiriki zoezi hilo licha ya kuwa
baadhi ya vyama vilitoa matamko ya kujitoa lakini baadhi yao
hawakukamilisha matakwa ya kujitoa hasa la kuwa na wadhamini
waliowadhamini kwani hawakudhaminiwa na makao makuu ya vyama vyao.
Katika zoezi hilo
vyama vyote vitashiriki licha ya kuwa hakuna idadi kamili ya vyamba
hivyo, lakini vyote vitashiriki na siku ya Jumanne tathmini halisi ya
vyama vingapi vilishiriki itatolewa.
0 comments:
Post a Comment