Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo,Prof. Siza Tumbo,akizungumza wakati akifungua kikao cha
uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na
biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti
za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza
Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Ushauri Elekezi
kutoka ESRF, Vivian Kazi,akitoa taarifa wakati wa kikao cha
uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na
biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti
za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza
Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Afisa Miradi kutoka AGRA, Liston
Njoroge,akiongea wakati kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu
kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi
uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa
kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya
Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya usalama wa
chakula kutoka wizara ya kilimo Dkt.Honest Kessy,akizungumza kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo,Prof.
Siza Tumbo,ambaye alifungua kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili
kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje
ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)
kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara
ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa kikao cha
uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na
biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi ya Tafiti
za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza
Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo,Prof. Siza Tumbo,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa
kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili kuhusu kuimarisha usalama wa
chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi uliofanywa na Taasisi
ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa kushirikiana na Taasisi ya
kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya Kilimo uliofanyika jijini
Dodoma.
………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Kilimo,Prof. Siza Tumbo amesema taarifa rasmi ya Benki ya Dunia
zinabainisha kuwa tayari Tanzania imeshafikia uchumi wa kati.
Prof.Tumbo ametoa kauli hiyo leo
jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha uwasilishaji wa tafiti mbili
kuhusu kuimarisha usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje
ya Nchi uliofanywa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) kwa
kushirikiana na Taasisi ya kuendeleza Kilimo Afrika (AGRA) na Wizara ya
Kilimo.
Amemshukuru Rais Dk.John Magufuli kwa kuiwezesha Tanzania kufikia na kujikita kwenye uchumi wa kati.
“Sasa hivi Tanzania tunachukuliwa
kama hatujafikia uchumi wa kati, naomba wataalam wetumjue kwamba
tumeshafikia uchumi wa kati sasa hayo maandishi kuwa tuna mpango wa
kufikia uchumi wa kati naomba mbadili, taarifa rasmi ya benki ya Dunia
imeshasema Tanzania ipo kwenye uchumi wa kati isipokuwa hatujajikita
katikati ya uchumi wa kati ndo tofauti.”amesema.
Hata hivyo, amebainisha kuwa kuna
wakati Tanzania iliingia uchumi wa kati lakini ikatereza na kwasasa
imerudi tena na kwamba uwezekano wa kuteleza ni mdogo.
“Kwasababu hizo napenda kumshukuru
Rais John Magufuli kwa kuweza kutuingiza kwenye uchumi wa kati na
tunaendelea kujikita kwenye uchumi wa kati, sasa hivi ukuaji wa uchumi
kwenye upande wa kilimo sasa hivi tumefikia asilimia 5.3 na lengo ni
asilimia 6 kwa hiyo tayari tunakwenda kwa kasi,”amesema.
Prof.Tumbo amesema kwa mwaka huu
Tanzania imefikia asilimia 109 ya utoshelevu wa chakula kwa kuwa na
ziada ya chakula tani milioni 2.5.
Akizungumzia kuhusu uuzaji mazao
nje ya nchi, Prof.Tumbo amesema kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia
Julai hadi Septemba mwaka huu, Tanzania imeuza nchini Burundi mihogo
tani 5,000 Burudi, tani 2000 za mtama na mahindi tani 84,000.5.
“Kwa kuwa tunahamasisha
mabadilishano ya kibiashara tumeingiza mahindi tani 56000.4, kwa hiyo
kimahesabu jumla ya tani zilizoenda nje ni tani 28,100 unaposema kwamba
unataka ku encourage trade ni pamoja na watu kuingiza vitu kwako na wewe
kupeleka nje ya nchi, mchele ndo tumeingiza kidogo sana tani
20,”amesema.
Kadhalika, amesema zao kubwa linaloingizwa ndani ya nchi ni ngano kutokana na uzalishaji kuwa chini.
Kwa Upande wake,Mkuu wa Idara ya
Ushauri Elekezi kutoka ESRF, Vivian Kazi amesema wamefanya kazi nyingi
za kitafiti na kwamba zinalenga kusaidia kuchangia ukuaji wa uchumi wa
Taifa pamoja na kuboresha usalama wa chakula kwa kupitia usimamizi bora
na madhubuti.
Amesema malengo ya mradi wa tafiti
hizo ni kuboresha upatikanaji wa taarifa,kuboresha mahusiano ya
kiutendaji na taasisi muhimu zenye majukumu ya kusimamia usalama na
biashara chakula,kuimarisha taratibu za tathmini za chakula ili
kuboresha makadirio kwa kuzingatia matokeo ya vipimo.
Naye, Afisa Miradi kutoka AGRA,
Liston Njoroge amesema wataendelea kushirikiana na taasisi hiyo na
serikali kufanya tafiti nyingi zaidi kwenye masuala ya kuimarisha
usalama wa chakula na biashara ya mazao ndani na nje ya Nchi ili kuleta
tija kwa Taifa.
0 comments:
Post a Comment