METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, November 23, 2019

Taasisi za Nunuzi Wamesisitizwa Kuandaa Mpango wa Ununuzi Ili Mahitaji Yapatikane kwa Wakati


Wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakiwa katika picha ya pamoja na Wawezeshaji wa seina hiyo eneo la Mtumba katika Mji wa Serikali leo jijini Dodoma mara baada ya kumaliza mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe hao juu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016 pamoja na  kanuni zake za mwaka 2013 ili wawe na usimamizi sahihi wa mikataba yenye kuleta tija na thamani bora ya fedha za Serikali.

(Picha na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma)
……………………

Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Dodoma

Wataalamu wa Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) wamesitiza Taasisi za Nunuzi  kuandaa vizuri mpango wa ununuzi na kusimamia utekelezaji wake ili mahitaji husika yaweze kununuliwa na kupatikana kwa wakati.


Akizungumza na wajumbe wa Bodi ya Zabuni ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo eneo la Mtumba katika Mji wa Serikali jijini Dodoma, Mwezeshaji wa mafunzo ambaye pia ni Afisa Ununuzi wa Umma kutoka (PPRA) Frank Yesaya amesema nia ya mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wajumbe hao juu ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2011 na marekebisho yake ya mwaka 2016 pamoja na  kanuni zake ili wawe na usimamizi sahihi wa mikataba yenye kuleta tija na thamani bora ya fedha za Serikali.


Frank ameongeza kuwa ni muhimu uwepo ushirikiano kati ya vyombo vinavyohusika na kufanya maamuzi na kutekeleza shughuli mbalimbali katika mchakato wa ununuzi wa umma.
Vyombo hivyo ni pamoja na mamlaka ya kuidhinisha bajeti, bodi ya zabuni, kitengo cha ununuzi, idara tumizi, Kamati  ya tathmini ya zabuni, timu ya majadiliano pamoja na kamati ya ukaguzi.


“Ni muhimu kushirikiana, kila mmoja atimize wajibu na majukumu yake bila kuingiliana hatua inayopelekea mchakato wa ununuzi kuwa wa tijakatika ofisi husika.” alisema Frank.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Idara ya Ununuzi na Ugavi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi Cecilia Kasonga amesema mafunzo yanasaidia kuwaimarisha katika kutekeleza majukumu yao ambapo ni vema mafunzo yatolewe mara kwa mara ili kurahisisha kazi na kuwapa fursa wajumbe wa bodi kujua taratibu za ununuzi wa umma hatua itakayosaidia kutoa maamuzi sahihi.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com