Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama
akizungumza wakati wa kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa
sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa
vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA Novemba 1,
2019 Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu
(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Bw. Andrew Masawe akizungumza
wakati wa ufunguzi wa kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa
sekta ya usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa
vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu
(Vijna na Ajira) Mhe. Antony Mavunde akitoa neno la shukrani wakati wa
kufunga kikao cha majadiliano kati ya Serikali na wadau wa sekta ya
usafirishaji wakiwemo kutoka vyama vya madereva na viongozi wa vyama vya
wamiliki wa vyombo vya usafirishaji ikiwemo TABOA kilichofanyika
Novemba 1, 2019 Dodoma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri
Mkuu Kazi,Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe Jenista Mhagama na Naibu
wake Mhe Antony Mavunde wakishuhudia zoezi la utiaji saini wa maazimio
ya kikao cha pamoja kati ya wadau wa sekta ya uchukuzi na Serikali
kilichofanyika Novemnba 1, 2019 Jijini Dodoma.
Viongozi wa vyama vya wa wamiliki
wa vyombo vya usafirishaji wakiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe
Jenista Mhagama kulia kwake ni Naibu wake Mhe.Anthony Mavunde na kushoto
kwake ni Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo (Kazi, Ajira, Vijana na Wenye
Ulemavu).
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
………………
NA; MWANDISHI WETU
Serikali ya Awamu ya Tano
imedhamiria kuendelea kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya
usafirishaji hapa nchini ili iweze kuongeza mchango wake katika kukuza
uchumi.
Akizungumza Novemba 1, 2019 Jijini
Dodoma wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Vyama vya Madereva na Vyama
vya Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali ni
kujenga mazingira wezeshi kati ya wadau wote wa sekta ya usafirishaji
hapa nchini wakiwemo madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji.
“Moja ya maazimio ya mkutano wetu
wa leo ni kuwataka wamiliki wa vyombo vya usafiri ambao hawajatoa mikata
ya ajira kwa madereva wao waanze kutoa mikataba ya ajira iliyoboreshwa
suala hilo lianze kutekelezwa mara moja kwa kuwa ni takwa la kisheria na
sio jambo la hiari” Alisisitiza Mhagama
Kutolewa kwa mikataba hiyo ni
matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa kati ya pande hizo mwaka 2017
yakitaka kuwepo kwa mikataba ya ajira iliyoboreshwa kwa madereva wote
itakayoleta ustawi wa maslahi ya pande hizo na Taifa kwa ujumla.
Alifafanua kuwa mkutano huo
umefanikisha kufikiwa kwa maazimio ya pamoja kati ya Serikali, wamiliki
na madereva kupitia viongozi wa makundi hayo ili kuchochea ustawi wa
sekta hiyo na kuondoa hali ya malalamiko na mapungufu yaliyobainika
katika ukaguzi uliofanyika mwezi Julai na Agosti 2019 kwa lengo la kuona
namna sheria za kazi zinavyozingatiwa.
Azimio jingine ni kuendelea kutoa
elimu kwa makundi hayo kupitia vyama vya wamiliki na madereva ili
kupunguza au kuondoa changamoto zilizopo hasa zilizoibuliwa katika
ukaguzi uliofanyika hivi karibuni.
Aidha, Waziri Mhagama ameviagiza
vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji kuhakikisha wanaruhusu
wafanyakazi kuanzisha matawi ya vyama vya wafanyakazi kwa Makapuni
ambayo hayajafanya hivyo bado.
“Vyama vya wafanyakazi vinasaidia
sana kuleta tija na ufanisi katika maeneo ya kazi maana wafanyakazi
hutumia vyombo hivyo kushauriana namna bora ya kutatua changamoto
zinazowakabili,” alisema Mhagama
Katika hatua nyingine Waziri
Mhagama aliwataka madereva na wamiliki wa vyombo hivyo kuendelea
kuzingatia sheria na kuthamini utu na heshima pande zote mbili, Serikali
itachukua hatua kwa yeyote atakayekiuka misingi hiyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri,
Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijna na Ajira Mhe. Antony Mavunde amesema
kuwa maazimio yaliyofikiwa katika mkutano huo yatasaidia kutatua
changamoto zilizoibuliwa na madereva na wamiliki wa vyombo vya
usafirishaji.
Mkutano wa wadau wa sekta ya
usafirishaji umefanyika Jijini Dodoma ukishirikisha Wizara zinazohusika
na masuala ya uckuzi na Ujenzi.
0 comments:
Post a Comment