Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo leo tarehe 9 Novemba 2019. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Sehemu ya wanachama wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Arusha Kurugenzi wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo leo tarehe 9 Novemba 2019.
Aliyekuwa Meneja wa Chama cha Ushirika cha Akiba na Mikopo cha Arusha Kurugenzi Christina Sumaye (Kulia) akiwa na aliyekuwa karani wa SACCOS hiyo Edith Malley wakifatilia hotuba ya Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) kabla ya kuagiza kukamatwa kwa viongozi hao wakati wa kikao kazi kilichofanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo Mhe Mrisho Gambo leo tarehe 9 Novemba 2019.
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Arusha
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) ameliagiza jeshi la Polisi Mkoani Arusha kwa
kushirikiana na Mkuu wa Upelelezi, na Kamanda wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana
na rushwa (TAKUKURU) kuwakamata viongozi mbalimbali wa Chama cha Ushirika cha
Akiba na Mikopo cha Arusha Kurugenzi kutokana na ubadhilifu wa fedha za
wanachama.
Waziri
Hasunga ametoa maagizo hayo leo tarehe 9 Novemba 2019 mara baada ya kusikiliza
malalamiko ya wanachama wa chama hicho wakati wa kikao kazi kilichofanyika
katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha na kuhudhuriwa pia na Mkuu wa Mkoa huo
Mhe Mrisho Gambo.
Amesema
kuwa watuhumiwa hao wanapaswa kukamatwa haraka iwezekanavyo kuanzia waliokuwa
viongozi mwaka 2004 mpaka 2015 ili kurudisha fedha zote walizozizihujumu za
wanachama na walizokopa.
Wengine
alioagiza wakamatwe ni pamoja na wajumbe wote wa kamati za mikopo, Kamati ya
usimamizi wa SACCOS iliyokuwepo kipindi chote hicho, Wajumbe wote wa Bodi ya
SACCOS iliyokuwepo awali kabla ya Bodi iliyopo sasa. “Tunachotaka sisi fedha
zote za wanachama zirudi na hata leo wakirudisha fedha hizo hatutaendelea na
kesi” Alisema
Pia
ameagiza mwanachama wa SACCOS hiyo Bi Zainab Nassor aliyeanzisha vikundi hewa
14 akamtwe, huku wengine ni aliyekuwa Mwenyekiti wa SACCOS Dkt Freedom
Makiago, Makamu Mwenyekiti Gasto Gasper, Meneja Christina Sumaye, na
wajumbe Andrea Sekidio, Joseph Kuhamwa na Mwanahamisi Gembe.
Katika
hatua nyingine Mhe Hasunga ameagiza kukamatwa kwa aliyekuwa Mwenyekiti wa
kamati ya Usimamizi Bi Mwanahawa Kombo, na wajumbe Samwel Mushy, Estomin
Chang’ah. Huku akiagiza pia karani wa SACCOS hiyo Edith Malley kukamatwa.
Katika
hatua nyingine ameagiza viongozi wote walioandikwa kwenye vikundi vya mikopo
kukamatwa haraka iwezekanavyo na kuchukuliwa hatua za haraka ikiwemo kurudisha
fedha za wanachama.
Mhe
Hasunga amesema kuwa lengo la kunzishwa vyama vya ushirika ilikuwa ni
kuwanufaisha wananchi kupitia umoja huo muhimu kwani mafanikio yanahusisha
nguvu ya pamoja.
Hata
hivyo ameagiza Bodi iliyopo madarakani kubainisha taarifa za kumbukumbu zote za
chama hicho kwa kuonyesha idadi ya wanachama na akiba walizonazo katika chama,
idadi ya hisa na kiasi cha fedha zinazodaiwa na kila mwanachama.
Kwa
sasa chama kinadaiwa fedha kiasi cha shilingi 2,486,365.68 zilizotokana
na mikopo kutoka Taasisi mbalimbali za kifedha, Amana, Akiba na Hisa za
wanachama hususani wastaafu ambazo zilichukuliwa kwa kutumiwa na wahusika hao
bila utaratibu na kwa malengo yao binafsi.
Wanachama
wastaafu wanadai zaidi ya shilingi 831,764,924.87 zitokanazo
na fedha za Amana walizoweka katika chama kutumia viinua mgongo vyao baada ya
kustaafu utumishi, Akiba na Hisa walizowekeza tangu wajiunge na chama hicho.
Wanachama
wanaoendelea na chama na waliojitoa wanadai zaidi ya shilingi 770,181,745.56 zitokanazo
na Amana, Akiba na Hisa walizowekeza tangu wajiunge na chama hicho.
Kadhalika,
Taasisi za kifedha zinazodai ni pamoja na (CRDB, NSSF na TUMAINI SACCOS)
wanaodai zaidi ya shilingi 874,575,517.25 bakaa ya mikopo
iliyotolewa bila kuzingatia utaratibu wa kifedha na kwa kutumia taarifa za udanganyifu.
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga yupo Mkoani Arusha kwa ziara ya kikazi ya siku 2
kwa mualikowa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo ambapo pamoja na mambo
mengine atashuhudia shughuli za sekta ya kilimo.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment