************************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam Mhe.
Paul Makonda leo November 23 amewaapisha Wajumbe Saba kati ya Nane wa
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Wilaya ya Kinondoni na Temeke na kuwaagiza
wajumbe hao kuhakikisha wanatumia elimu na utaalmu wao kutatua Kwa
haraka tatizo la Migogoro ya Ardhi ambalo limekuwa kero kwa Wananchi.
RC Makonda amesema moja ya mambo
yanayomnyima usingizi ni pale anapoona Wajane, Wazee, Yatima na Watu
wasiokuwa na elimu ya kutosha wanapokonywa haki zao na “Wajanja” wenye
uelewa wa Sheria ambapo amewaka wajumbe hao kutazama suala hilo kwa
jicho la Tatu.
Aidha RC Makonda amewataka Wajumbe
hao kuepuka tabia ya kukaa maofisini na kusubiri wananchi na badala
yake watoke nje wakashugulike matatizo ya watu.
Pamoja na hayo RC Makonda
amewataka wajumbe hao wahakikishe Wanatumia Hekima na Busara kumaliza
migogoro pamoja na kuhakikisha Mashauri hayakai muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment