Saturday, November 23, 2019

RC MAKONDA AWAAPISHA WAJUMBE WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA, AWATAKA WATUMIE ELIMU YAO KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI NA SIO KUKANDAMIZA WANANCHI

 

************************************

Mkuu wa Mkoa wa Dar ea salaam Mhe. Paul Makonda leo November 23 amewaapisha Wajumbe Saba kati ya Nane wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Wilaya ya Kinondoni na Temeke na kuwaagiza wajumbe hao kuhakikisha wanatumia elimu na utaalmu wao kutatua Kwa haraka tatizo la Migogoro ya Ardhi ambalo limekuwa kero kwa Wananchi.


RC Makonda amesema moja ya mambo yanayomnyima usingizi ni pale anapoona Wajane, Wazee, Yatima na Watu wasiokuwa na elimu ya kutosha wanapokonywa haki zao na “Wajanja” wenye uelewa wa Sheria ambapo amewaka wajumbe hao kutazama suala hilo kwa jicho la Tatu.

Aidha RC Makonda amewataka Wajumbe hao kuepuka tabia ya kukaa maofisini na kusubiri wananchi na badala yake watoke nje wakashugulike matatizo ya watu.

Pamoja na hayo RC Makonda amewataka wajumbe hao wahakikishe Wanatumia Hekima na Busara kumaliza migogoro pamoja na kuhakikisha Mashauri hayakai muda mrefu.

No comments:

Post a Comment