Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine Shigela akitoa hotuba kwa wadau wa kongomano la ukatili dhidi ya watoto leo Mkoani Tanga.
Badhi ya viongozi wa dini wa Mkoa
wa Tanga wakiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw.
Martine Shigela wakati wa kongomano la ukatili dhidi ya watoto leo
Mkoani Tanga.
Badhi ya wanafunzi kutoka shule
mbalimbali za Mkoa wa Tanga wakifuatilia jambo wakati wa kongomano la
ukatili dhidi ya watoto leo Mkoani Tanga.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya
Watoto kutoka Wizara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bw. Sebastian
Kitiku akifafanua jambo kuhusu ukatili wa watoto mitandaoni wakati wa
kongomano la ukatili dhidi ya watoto leo Mkoani Tanga.
……………..
Na mwandishi wetu TANGA.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga Bw. Martine
Shigela amekemea tabia ya Wazazi, Walezi pamoja na Jamii ya Mkoa wa
Tanga kukumbatia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto jambo ambalo
linasababisha mkoa huo kuwa na takwimu za juu za vitendo vya ukatili
kuliko mikoa mingine.
Mkoa wa Tanga kwa mujibu wa
takwimu za jeshi la Polisi hapa Nchini unaongoza kwa vitendo vya ukatili
dhidi ya watoto ndio maana Wizara ya Afya pamoja na wadau wameamua
kuweka kongamano la vitendo vya ukatili dhidi ya watoto mkoani humo ili
kujadiliana namna bora ya mkoa huo kuondokana na changamoto hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga katika
hotuba yake kwa wadau wa kongomano hilo amesema ni vitendo vya haibu kwa
wakazi wa mkoa huo kuendelea kutajwa kuhusiana na ukatili dhidi ya
watoto na hivyo kuwataka wadau wa kongamano hilo kuja na mkakati
utakaowezesha mkoa huo kuweka mikakati ya kupambana na hatimaye
kutokomeza kabisa ukatili dhidi ya watoto mkoani humo.
Aidha Mkurugenzi wa Watoto Wizara
ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii Bi. Mwajuma Magwiza amesema
kimsingi Kongamano hilo linafanyika Mkoani Tanga kutokana na Mkoa huo
kuongoza kwa vitendo vya ukatili hapa Nchini akiongeza kuwa kongamano
hilo linahusisha watoto, viongozi wadini na wazee mashuhuri wa mkoa huo
ili kwa pamoja kutafuta namna bora ya kutokomeza vitendo hivyo.
Aidha Bi. Magwiza ameviambia
vyombo vya habari kuwa Kongamano hilo lianaangazia changamoto ya ukatili
dhidi ya watoto kama janga kubwa ambalo kimsingi halinabudi kuangaliwa
upya kwa mustakabali wa ustawi wa maisha ya baadae ya mtoto.
Bi. Magwiza ameyataja maeneo manne
ambayo Wizara yake na wadau watatotoa kwa ajili kuelimisha Kongamano
hilo kuwa ni eneo la ukatili kwa ujumla wake, wajibu wazazi na walezi
katika makuzi ya mtoto,ukatili wa watoto mtandaoni pamoja na umuhimu wa
malezi na makuzi kwa ajili ya maendeleo ya mtoto.
Wakati huo huo Mkurugenzi Msaidizi
Idara ya Watoto kutoka Wiazara ya Afya Idara Kuu Maendeleo ya Jamii
Bw. Sebastian Kitiku akifafanua zaidi kuhusu ukatili wa watoto
mitandaoni ameonya wazazi na walezi hapa Nchini kuwa makini na watoto
wakati wa matumizi ya vifaa vya kielektroniki kwani vifaa hivyo
vinatumika katika kuendeleza vitendo vya ukatili dhidi ya watoto.
Bw. Kitiku ameliambia kongamano
hilo kuwa watoto ni weledi sana katika matumizi ya simu pamoja na
television za kisasa na wanatumia muda mwingi katika vifaa hivyo
akizitaja simu kuwa tishio kwani watoto wanapata ukatili wa kingono
mtandaoni kupitia mawasiliano ya simu na kompyuta na kupelekea wengine
kujiua baada ya kukosa usaidizi baada kufanyiwa ukatili na watu wasio
wajua.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kila ifikapo leo tarehe 20 Novemba
uungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Haki
za Mtoto pamoja na kusherehekea miaka 30 ya utekekelezaji wa Mkataba wa
Kimataifa wa Haki za Mtoto ndiyo dhana ya kongamano hili ambalo
limefanyaika leo ili kutoa fursa kwa wadau wengi zaidi kushiriki
kuadhimisha siku hii.
Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa
Haki za Mtoto ulipitishwa rasmi na nchi wanachama wa umoja huo mnamo
tarehe 20 Novemba, 1989 sambamba na uanzishwaji wa Mkataba wa Kimataifa
wa Haki za Mtoto (Child Rights Convention) ambapo hadi sasa nchi 190 wanachama wa Umoja wa Mataifa ambazo zimetia saini na kuridhia mkataba huu.
0 comments:
Post a Comment