Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga
(Mb) akizungumza na waandishi wa habari Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini
Dodoma kuhusu ubadhilifu alioubaini kwenye malipo ya wakulima wa korosho. Wengine pichani ni Naibu Mawaziri wa Kilimo Mhe Omary Mgumba (Kulia) na Mhe Hussein Bashe (Kushoto) (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya
Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma kuhusu ubadhilifu alioubaini kwenye malipo ya wakulima wa korosho.
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) akizungumza na waandishi wa habari Ofisi ndogo ya Wizara ya Kilimo Jijini Dodoma kuhusu ubadhilifu alioubaini kwenye malipo ya wakulima wa korosho.
Dodoma, 17 Novemba,
2019
Ndugu Wanahabari;
Kama mnavyofahamu, Mhe. Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alitoa maelekezo ya kuwa
katika msimu wa korosho wa mwaka 2018/2019 kuwa Serikali itanunua korosho zote
za Wakulima ili kuwaondoa kwenye kusuasua kwa bei ya korosho.
Tarehe 12/11/2018 Wizara ya Kilimo kupitia
Bodi ya Mazao Mchanganyiko na Bodi ya Korosho Tanzania ilianza kutekeleza agizo
la Mhe. Rais kwa kuunda Kamati Maalum ya kusimamia zoezi la ununuzi wa korosho ghafi
kutoka kwa Wakulima wa mikoa ya Pwani, Lindi Mtwara na Ruvuma.
Jumla ya korosho zote zilizokusanywa
zilikuwa ni tani 222,561.1 zenye thamani ya Shilingi Bilioni 732.8. Korosho hizo
zilikuwa za madaraja mawili ambayo ni daraja la kwanza (Standard grade) tani
204,476.1 zenye thamani ya Shilingi
674,522.700 na daraja la pili (Under grade) tani 18,084.9 zenye thamani ya
Shilingi Bilioni 47,744,294,400. Hadi sasa Serikali tayari imelipa kwa
wakulima jumla ya Shilingi Bilioni 707.8
sawa na tania 217,786 za korosho ghafi.
Aidha,hivi karibu Mhe.Rais Magufuli
aliagiza Wizara ya Fedha kutoa Shilingi Bilioni 40 kwa ajili ya kuwalipa
wakulima na watoa huduma wengine waliokuwa wanadai malipo yao ya korosho msimu
wa 2018/2019.
Ndugu
Wanahabari;
Nimewaita ili niwafahamishe kwa nini hadi
leo hatujakamilisha zoezi la kuwalipa wakulima hao kutokana na sababu kadhaa:
Kwanza; imeonekana kuwa kuna udanganyifu
mkubwa ambao umefanywa na Viongozi wa Vyama vya Msindi katika mkoa wa Pwani.
Mfano Chama cha Msingi cha (Sanga Sanga AMCOS) katika msimu uliopita; walikusanya
kilo 212 tu lakini kwenye hesabu imeonekana walifanya udanganyifu na kuongeza
kilo elfu saba zaidi (7,000). Aidha, walitoa
taarifa ya uongo kuhusu uwepo wa korosho za daraja la kwanza za kilo 244 badala
ya daraja la pili, udanganyifu huo, ulisababisha Serikali kulipa zaidi ya shilingi
Milioni 222,328,867 kwenye Chama
hicho cha Msingi (Sanga Sanga AMCOS).
Mfano mwingine, katika mkoani Mtwara,
wilaya ya Tandahimba. Timu ya Uhakiki ya
Wizara iligundua malipo hewa ya Shilingi Bilioni
1.6. Wizara ya Kilimo tumepata
wasiwasi na kutilia shaka mwenendo wa uadilifu wa baadhi ya Viongozi wasio
waaminifu. Tumeamua kuchukua hatua ili
tujiridhishe kabla ya kufunga msimu wa ununuzi wa korosho wa mwaka 2018/2019.
Ndugu
Wanahabari,
Kutokana na mapungufu hayo, nimeamua kuunda
Timu ya Uchunguzi ya watu watano (5) ili washirikiane na Timu ya uhakiki ya
Wizara ya Kilimo kwa ajili ya uchunguzi wa kina wa mwenendo mzima wa biashara
ya korosho kwa msimu wa 2018/2019. Timu
zote mbili zitafanya kazi kuanzia sasahadi tarehe 15 Januari, 2020.
Pili, Timu ya Uchunguzi; itatakiwa
kuhakiki majina ya Wakulima kutoka kwenye Vyama vya Msingi, kwenda Vyama Vikuu
na baadae Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko kwenda kwenye mfumo wa malipo ya
Benki ili kubaini fedha walizolipwa Wakulima zililipwa kupitia, akaunti zao.
Tatu, Timu ya Uchunguzi; itatakiwa
kuchunguza kama kulikuwa na unyaufu kwenye korosho zote, zilizonunuliwa kwenye msimu
wa 2018/2019 na kama unyaufu ulikuwepo, ulikuwa ni wa kiwango gani ili Serikali
itoe taarifa inayoendana na uhalisia.
Ndugu
Wanahabari;
Aidha, mtakumbuka kuwa Desemba, 2016
Serikali iliamua kuufuta Mfuko wa Wakfu wa Maendeleo ya zao la Korosho
(Cashewnut Development Trust Fund - CDTF) na baadae majukumu yake, yalikasimiwa
na Bodi ya Korosho, wakati Mfuko huo unafutwa ulikuwa na fedha taslimu Benki
shilingi Bilioni 53.2. Fedha hizo kazi yake ilikuwa kuendeleza tasnia
ya korosho ambapo jukumu kubwa lilikuwa ni kujenga viwanda vitatu vya kubangua
korosho na ujenzi wa ghala la kuhifadhia korosho. Viwanda hivyo vilikuwa vijengwe eneo la Mkinga
(Tanga), Mkuranga (Pwani) na Tunduru (Ruvuma).
Jambo la kusikitisha ni kuwa, Bodi ya
Korosho ilishindwa kutekeleza majukumu hayo ya kujenga viwanda hivyo na ghala
badala yake fedha hizo zilitumika kinyume na makusudio. Jambo baya zaidi kuna
viashiria ambavyo vinatia shaka na kutoa tahadhari ya kufanyika kwa haraka kwa
uchunguzi wa kina wa namna fedha hizo zilivyotumika. Viashiria hivyo ni pamoja
na matumizi ya zaidi ya shilingi milioni
600 zilizotumika kwa ajili ya kulipia gharama za uandaaji wa mikutano ya
Wadau, pamoja na malipo ya pembejeo kiasi cha zaidi ya Bilioni 28 na malipo kwa Watoa huduma (Wauzaji wa magunia). Malipo
ya shilingi Bilioni 12 ambayo
yameonekana, yalishalipwa kwa watoa huduma hao.
Malipo mengine tunayotilia mashaka ni
pamoja na Bodi ya Korosho kuvilipa Vyama Vikuu vya TANECU Bilioni 1.8, CORECU Bilioni
2.1 kwa maelezo kuwa hayo ni madai ya miaka iliyopita ambapo Bodi ya
Korosho ilikuwa ikidaiwa.
Ndugu
Wanahabari;
Nimalizie kwa kusema, baada ya kuona kuna
viashiria na mwenendo usioridhisha, naelekeza kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) kufanya uhakiki na uchunguzi ili kuangalia namna kiasi cha fedha
cha shilingi Bilioni 53.2
zilivyotumika na kama itabainika, wale wole waliohusika na matumizi mabaya ya
fedha hizo za umma wachukuliwe hatua kwa mujibu ya sheria za nchi.
Japhet Hasunga (Mb)
WAZIRI
WA KILIMO
0 comments:
Post a Comment