Kaimu Msajili wa viuatilifu
Tanzania Dr Joseph Bukalassa amepiga marufuku kitendo cha
uuzaji na usambazaji wa viuatilifu bandia,vilivyoisha muda wake na
ambavyo havijakaguliwa na kusajiliwa kitendo ambacho amesema kinasababisha
kuwepo kwa madhara kwa watumiaji,mimea na mazingira kwa ujumla.
Bukalassa ameyasema
hayowakati wa kufunga mafunzo ya 51 ya matumizi sahihiu na salama ya viuatilifu
yaliyotolewa kwa wadau waviuatilifu(wauzaji,wakulima,maafisa ugani wa serikali
na wa sekta binafsi pamoja na wasambazaji wa viuatilifu)yenye lengo la
kuwawezesha wafanyabiashara wa viuatilifu kutekeleza majukumu yao ya kibiashara
kikamilifu ili waweze kuhudumia wateja wao kikamilifuna kuhakikisha kwamba
maswala muhimu yanazingatiwa.Kuwahudumia wateja wao na kuwataarifu ni kiambato
ganicha kiuatilifu kipo kwenye kiuatilifu hicho na kinafanya kazi gani pamoja
na namna bora na salama ya kutumia kiuatilifu hicho ili waweze kuwasadaidia
wale wanaoenda kupuliza moja kwa moja shambani
Aidha amesema kuwa kuuza na kusambaza
viuatilifu visivyo sajiliwa ,bandia vilivyoisha muda wa matumizi au kufanya
biashara ya uuzaji na usambazaji wa viuatilifu pasipo kukaguliwa na kusajiliwa
ni sawasawa na kujiingiza kwenye mtego usio teguka
“Vibali vyote hapa nchini
husauiniwa na mimi sasa kunatabia ukiona wakaguzi wanahitaji kuklagua duka lako
unawakimbia sasa mimi nisaini kibali chako alafu watu wangu unawakimbia
inamaanisha kuwa hufai kufanya biashara hapa nchini usiingie kwenye huo mtego
nakuhakikishia hautauza tena”amesema Dr Bukalassa
Kwa upande wake muwakilishi wa kaimu
mkurugenzi mkuu TPRI,Dr Ester Kimaro ambae pia ndo alikuwa mgeni
rasmi katika katika ufungaji wa mafunzo hayo amesemakuwa wafanyaji biashara za
viuatilifukuzingati sheria za nchi kama zilivyo biashara nyingine.
Aidha ameongeza kuwa matumizi ya
viuatilifu au biashara za viuatilifu zinaweza kusababisha madhara mbalimbali ya
kiafya kwa watumiaji,jamii,wanyama na hata mazingira kwa ujumla kama zikifanywa
bila kufuata taratibu na kanuni za matumizi sahihi ya viuatilifu
hivyo,amewataka wahitimu wa mafunzo hayo kupeleka elimu waliyoipata kwa wiki
mbili ya matumizi sahihi na salama ya matumizi ya viuatilifu na udhibiti
endelevu wa visumbufu kwa jamiii ili kuepuka kuwepo kwa madhara hayo.
Pia amesemakuwa ni matarajio wa
taasisis hiyo kuwa kutokana na elimu waliyo ipata watakwenda kuhamasisha
matumizi sahihi na salama ya matumizi ya viuatilifu na udhibiti endelevu wa
visumbufu ikiwemo kutokomeza uuzaji na usambazaji wa viuatilifu visivyo
kaguliwa na sajiliwa na TPRI.
Amesemakuwa washiriki wa mafunzo hayo
watakuwa na uwezo wa moja kutambua viuatilifu bandia,vilivyoisha muda wake na
visivyo sajiliwa,mbili kutambua,kuainisha na kudhbiti magonjwa na wadudu wa
mimea ya kilimo pamoja na wadudu waenezao magonjwa kwa binadamu na mifugo,tatu
kujua aina mbvalimbali za mabomba na stadi za kutumimia mabomba ya unyunyuziaji
viuatilifu,nne kujua aina mbalimbali za viuatilifu, kutambua athari za
viuatilifu kwa binadamu,mifugo,mimea na mazingira.
Pia tano kusoma,kutasfiri mambo yote
yaliyoandikwa kwenye vibandiko hivyo kuwasaidia kutoa maelekezo kwa watumiaji
wa viuatilifu hususani wakulima,sita kujua namna ya kusajili biashara ya
viuatilifu kwa njia rafiki na rahisi popote kwa kutumia teknolojia ya mtandao
yaani ATMIS, sita kufanya biashara za usambazaji na uuzaji wa viuatilifu
kikamilifu bila kuvunja sheria na ufukizaji wa mazao.
Kwa mujibu wa Bw Jumanne
Rajabu mchambuzi mfawidhi wa viuatilifu ambae pia ndiye mratibu wa
mafunzo hayo amesemakuwa mafunzo hayo yataleta tija katika Kilimo kwani
wahitumu walio hitimu watakwenda kutoa huduma sahihi na salama kwa wakulima.
Aidha ameongezakuwa mafunzo hayo
yanaendeshwa TPRI makao makuu Arusha kila wiki ya pili ya mwezi wa tano na kila
wiki ya pili ya mwezi wa kumi na moja kila mwaka kwa wiki mbili na mikoani
ambapo hufanyika kwa wiki moja hivyo ametoa wito kwa wauzaji,wakulima,maafisa
ugani wa serikali na wa sekta binafsi pamoja na wasambazaji wa viuatilifu
kuhudhuria wanaposikia kunamafunzo mikoani na hayo yanayo fanyikia makao makuuu
Arusha.
Amemalizia kwa kusemakuwa sheria
inawataka wauzaji na wasambazaji wa viuatilifu kupata mafunzo kabla ya kuanza
kufanya biashara hivyo amewaasa wanaotaka kufunzgua biashara hivyo ili
waepukane na usumbufu kutoka kwa mamlaka yaani wakaguzi wa biashara za
viuatilifu wa mara kwa mara wafike kupata mafunzo na vyete ambavyo vitawasaidia
kwenye kufanya usajili wa biashara zao.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment