
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo
Oktoba 20, 2019 ameondoka chini kwenda Urusi ambako atamwakilisha Rais
Dkt.John Pombe Magufuli katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa
Afrika na Urusi. Pichani, Waziri Mkuu akisalimiana na Spika wa Bunge Job
Ndugai kwenye Uwanja Ndege wa Julius Nyerere kabla ya kuondoka. (Picha
na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
anaondoka nchini leo (Jumapili, Oktoba 20, 2019) kwenda Urusi kuhudhuria
mkutano baina ya Wakuu wa Nchi na Serikali kutoka mataifa ya Afrika na
Urusi (Russia-Africa Summit), utakaofanyika jijini Sochi, Urusi, Oktoba
23 – 24, 2019.
Waziri Mkuu anahudhuria mkutano huo kwa niaba ya Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli.
Mkutano huo utakaoendeshwa
chini ya uenyekiti wa pamoja (Co-chaired) wa Rais wa Shirikisho la
Urusi, Vladimir Putin, na Rais wa Misri, Abdel Fattah el-Sisi, ambaye
pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), unalenga kurejesha na
kuimarisha uhusiano baina ya mataifa ya Afrika na Urusi ambao uliyumba
baada ya kusambaratika kwa “Union of Soviet Socialist Republic” (USSR)
mwaka 1991.
Mkutano huo wa Wakuu wa Nchi
na Serikali utafanyika katika sehemu mbili, ambazo ni Kongamano la
Biashara (Russia Business Forum) linalotarajiwa kufanyika Oktoba 23, na
Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Urusi na Afrika uliopangwa
kufanyika Oktoba 24, 2019.
Waziri Mkuu atashiriki kwenye mikutano yote miwili.
0 comments:
Post a Comment