
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza na Watumishi wa
sekta ya ardhi wa halmashauri za Wilaya na Mji za mkoa wa Geita jana
wakati wa ziara yake ya kuangalia utendaji wa sekta ya ardhi katika mkoa
wa Geita.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akikagua Mradi wa ujenzi wa
Ofisi na Nyumba za Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) wilayani Chato mkoa wa Kagera wakati akikagua miradi ya ujenzi
inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC). Kulia ni Mkuu wa
wilaya ya Chato Charles Kabeho na kulia kwa Naibu Waziri ni Mhandisi wa
ujenzi wa Mradi huo Renatus Mhada.

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula pamoja na Mkuu wa Wilaya ya
Chato mkoa wa Kagera Charles Kabeho akielekea kukagua Mradi wa ujenzi wa
Ofisi na Nyumba za Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania
(TFS) wilayani Chato mkoa wa Kagera wakati akikagua miradi ya ujenzi
inayosimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
……………………..
Na Munir Shemweta, WANMM GEITA
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba
na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula amezitaka halmashauri nchini
kuhakikisha zinalinda maeneo yote ya hifadhi yaliyoidhinishwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli kuwa vijiji ili
yasiendelee kuvamiwa.
Dkt Mabula alitoa kauli hiyo
jana alipozungumza na watendaji wa sekta ya ardhi wakiwemo wakurugenzi
wa halmashauri za mkoa wa Geita wakati wa ziara yake ya siku moja
kutembelea mkoa huo kuangalia utendaji kazi wa sekta ya ardhi pamoja na
kufuatia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mwezi Machi 2019.
Alisema, ni jukumu la
halmashauri za wilaya wakati zikisubiri kuletewa tarifa rasmi ya maeneo
yaliyoidhinishwa kuwa vijiji na mengine yaliyobadilishiwa matumizi
kuyalinda maeneo hayo yasivamiwe tena ili taarifa itakapokwenda katika
halmashauri husika kuhusiana na maeneo pasiwepo uvamizi mwingine zaidi
ya ule wa awali kabla ya kutembelewa na timu ya Mawaziri nane.
Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, halmashauri ambazo maeneo yake ya
hifadhi yalivamiwa na vijiji vyake kuidhinishwa zitapelekewa taarifa
sambamba na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali vijiji
vilivyidhinishwa.
‘’Mna jukumu kulinda maeneo
hayo yasivamiwe tena kwa sababu kamati ya mawaziri wanne walipita kwenye
baadhi ya maeneo na yaliainishwa na kinachotakiwa kwenu ni kuhakikisha
hakuna uvamizi unaoendelea katika hifadhi ’’ alisema Dkta Mabula.
Alisema, Wizara ya Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi ishamaliza kupanga maeneo ya vijiji
yaliyoidhishwa mkoa kwa mkoa na kinachofanyika sasa ni kutangazwa katika
Gazeti la Serikali ili wananchi waweze kuishi kwa amani katika maeneo
hayo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dorothy Mwanyika wakati
wa kikao hicho na watendaji wa sekta ya ardhi alisema wizara yake katika
kukabiliana na upungufu wa watumishi wa sekta hiyo imejipanga
kuhakikisha inawagawa watumishi wa sekta ya ardhi waliopo katika
halmashauri kulingana na idadi iliyopo sasa.
Mwanyika alisema Wizara ya
Ardhi ina mahitaji ya watumishi wa sekta ya ardhi katika halmashauri
zote wapatao 2900 ambapo kwa sasa kuna jumla ya watumishi 1500 hivyo
kufanya kuwepo pungufu ya watumishi 1400. Hata hivyo, Katibu Mkuu huyo
wa Wizara ya Ardhi alisema, kinachofanyika sasa sasa kwa Wizara yake ni
kutambua watumishi waliopo na baadaye kuwatawanya katika mgawanyo mzuri.
Naye Kamishna Msaidzi wa Ardhi
Kanda ya Ziwa Makwasa Biswalo alisema halmashauri ambazo hazina
wataalamu wa kutosha zinazoazima kutika mikoa iliyo jirani na
halmashauri hizo wataalamu wake wa sekta ya ardhi wanatakiwa kufanya kwa
weledi na si vinginevyo ili kazi ya sekta hiyo iweze kwenda vizuri.
Katika hatua nyingine Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula
alikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa ujenzi wa Ofisi na Nyumba za
Watumishi wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) uliopo wilayani Chato
mkoani Kagera.
Akiwa katika ukaguzi wa mradi huo
unaogharimu Bilioni 1.2 na kusimamiwa na Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) Dkt Mabula alilitaka Shirika la Nyumba la Taifa kuhakikisha
linakamilisha ujenzi wa mradi huo katika muda uliopangwa kwa kuwa
shirika hilo sasa limeamiwa na serikali kwa kupatiwa miradi mbalimbali
nchini.
0 comments:
Post a Comment