
Mwenyekiti wa chama cha CODEPATA
Bw. Sunday Wambura akitoa hotuba yake wakati akizungumza na wanachama wa
chama hicho wakati wa Mkutano Mkuu wa chama uliofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo
ya Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bw. Patrick golwike akizungumza na Wananchama wa Chama cha
Wataalam wa Maendeleo ya Jamii nchini wakati Mutano wa Mwaka wa chama
hicho uliofanyika jijini Dodoma.

Baadhi ya wanachama wa CODEPATA
wakifuatilia kwa makini kuhusu maendeleo ya chama chao wakati wa
majumuhisho ya chama chao jijini Dodoma.

Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya
Jamii kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bw. Badru Abduburu (kushoto) akiokea cheti cha Shukrani kwa niaba ya
Wizara kutoka kwa Mwenyekiti wa chama cha CODEPATA Bw. Sunday Wambura
(kulia) mara baada ya kumalizika kwa kwa Mkutano wa Wataalam hao jijini
Dodoma.

Baadhi ya wadau
walioshirikiana na Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kufanikisha
mkutano wakiwa katika picha ya oamoja mara baada ya kupokea vyeti vya
shukrani kutoka katika Chama hicho mara baada ya kumalizika kwa Mkutano
wa Wataalam hao jijini Dodoma.
Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini WAMJW
************************
Na Mwandishi Wetu Dodoma
Wataalam wa
Maendeleo ya Jamii nchini wameaswa kutumia mbinu walizonazo kuleta
ushawishi kwa wnanchi na kuwahamasiha katika kujitolea kushiriki katika
shughuli za kimaendeleo katika maeneo yao.
Hayo yamebainika
jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Wataalam wa Maendeleo ya
Jamii uliwakutanusha Wataalam hao utoka Sekta za umma, Binafsi na
Mashieika Yasiyo ya Kiserikali nchini.
Akizungumza
wakati wa kikao hicho Rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii
CODEPATA Bw. Sunday Wambura amesema kuwa Maendeleo ya Jamii ni mchakato
unaowezesha watu kubadili fikra hasi kuwa chanya kuhusiana na maendeleo
yao katika nyanja zote.
Bw. Wambura
aliongeza kuwa Maendeleo ya Jamii ni mchakato kwa sababu huu unawezesha
watu kutambua uwezo walio nao wa kubaini matatizo na kutumia fursa na
rasilimali zilizopo kuboresha maisha kukuza kipato na uchumi wao kwa
ujumla.
Aidha Bw. Wambura
alieleza kuwa maendeleo endelevu na jumuishi yanasisitiza ushiriki wa
jamii katika kuamua, kupanga, kutekeleza, kufuatilia na kutathimini na
ili jamii iweze iwe na mtizamo chanya, kushiriki na kupokea mabadiliko
anwai inahitaji ulaghabishi.
“Wataalam wa
maendeleo ya jamii wanazo stadi za kutumia mbinu shirikishi
zinazowezesha kuamsha ari ya jamii kushiriki katika maendeleo yao
ikihusisha watu wote na makundi mbalimbali yaliyosahaulika katika jamii”
aliisitiza Bw. Wambura.
Bw. Wambura
amewakumbusha wanachama wa COPEDATA kuwa wataalum wa taaluma mbalimbali
duniani hujipambanua kupitia vyama vya kitaaluma na kuongeza kuwa uwepo
wa vyama hivi umekuwa na tija kwa uimara na ubora wa taaluma husika
pamoja na maendeleo ya Taifa kutokana na mchango wa vyama hivyo.
Bw. Wambura
alisema kuwa ni jambo la tija kwa Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuwa na
chama cha kitaaluma kinachowaunganisha na kuwaongoza akiongeza kuwa
chama chake bado ni kichanga kwahiyo kinahitaji hivyo kila mwanachama
anaowajibu wa kukijenga.
“Mwelekeo wa
Chama kuwa ni kuwa chama imara na chenye nguvu si kwa ajili ya kukinzana
au kupambana na mamlaka au taasisi yoyote bali kwa ajili ya kulinda ,
kutetea na kuweka viwango bora vya utendaji kazi vya Wataalam wa
Maendeleo ya Jamii’’. Aliongeza Bw. Wambura.
Wataalamu wa
Sekta ya Maendeleo ya Jamii wamemaliza Mkutano Mkuu wao wa mwaka Jijini
Dodoma uliolenga kukumbushana majukumu yao lakini pia kupata maarifa
mapya kutoka mada mbalimbali zitakazotolewa katika mkutano huo wa siku
nne.
0 comments:
Post a Comment