UZALISHAJI katika kiwanda cha saruji cha Dangote kilichopo Mtwara umesimama kwa muda kutokana na hitilafu za kiufundi zilizojitokeza katika mitambo.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa Dangote Tanzania, Harpreet Duggal alisema jana kwamba
mafundi wa Dangote wapo kazini na shughuli za uzalishaji zitarejea
katika siku chache zijazo.
Alisema
kiwanda kinachomilikiwa na bilionea namba moja Afrika, Alhaji Aliko
Dangote wa Nigeria kilianza uzalishaji wa kibiashara mwaka huu na kama
ilivyo kwa kiwanda kingine kama hicho, jambo lolote linaweza kutarajiwa
hasa katika miezi ya mwanzo.
Alisisitiza, “hitilafu hizi ni za kawaida na uzalishaji utarejea katika kipindi kifupi kijacho.”
Akizungumzia
gharama za uzalishaji, Duggal alisema uendeshaji nchini uko juu huku
miongoni mwa sababu ikiwa ni matumizi ya jenereta za dizeli katika
kuendesha kiwanda.
Hata hivyo, alisema serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kuwapunguzia mzigo.
0 comments:
Post a Comment