*****************************
Wakandarasi wa
Kampuni za CHICCO Engineering na Nyanza Road Work leo wamekamatwa na
Jeshi la Polisi Kanda maalumu ya Dar es salaam kwa agizo la Mkuu wa Mkoa
wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda ambae ameagiza kukamatwa kwa
wakandarasi hao kwa kosa la Kushindwa kutekeleza miradi ya Ujenzi wa Mto
Ng’ombe na Barabara ya Kivule kwa wakati na kuleta usumbufu Mkubwa kwa
wananchi ukiwemo wa Mafuriko, Nyumba Kubomoka, Uharibifu wa Mali, Ajali
na Magari kuharibika huku wakandarasi hao wakila Maisha mitaani.
Kwa mujibu wa RC
Makonda Mkandarasi wa Kampuni ya CHICCO amekamatwa kwa kushindwa kuanza
Mradi wa ujenzi wa Mto Ng’ombe unaogharimu Shilingi Bilioni 32 ambapo
licha ya Kusaini Mkataba Mkandarasi huyo hajaanza kazi kwa zaidi ya
Miezi minne na hadi sasa amelipwa zaidi ya Shilingi Bilioni 4.8 huku
wananchi wakiteseka na kero ya Mafuriko.
RC Makonda amesema
jambo hilo ni uzembe na hujuma inayoweza kuchonganisha Wananchi na
Serikali yao ambayo tayari imetoa fedha za ujenzi wa Mto huo ili
kuwaondolea kero lakini Mkandarasi amekuwa akisuasua kuanza kazi.
Kwa upande wa Kampuni
ya Nyanza RC Makonda ameagizwa kukamatwa kwa Mkandarasi huyo kwa
kushindwa kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Kivule na Daraja licha ya
Kupokea fedha zaidi ya Shilingi Milioni 800 jambo linalopelekea wakazi
wa Kivule kuteseka na kero ya ubovu wa Barabara na wakati mwingine
kusababisha Ajali na Kuharibika kwa Vyombo vya usafiri.
Kwa Maelekezo ya RC
Makonda Wakandarasi hao waliokamatwa watakuwa Wakilala Polisi Central na
asubuhi watatokea polisi kwenda kufanya kazi ya Ujenzi hadi hapo
atakapojiridhisha kuwa kazi inaenda vizuri huku akieleza kuwa zoezi hilo
la ukamataji litakuwa endelevu kwa Wakandarasi wote wanaokwamisha
miradi ya serikali.
0 comments:
Post a Comment