Nchi
ya Burundi imeishutumu Rwanda kwa madai ya kupanga kufanya majaribio ya
kutaka kumuua msaidizi wa Rais Pierre Nkurunziza, Willy Nyamitwe.
Msemaji
wa jeshi la polisi kutoka Burundi, Pierre Nkurukiye amesema maagizo ya
kufanywa kwa jaribio hilo lililofeli, yalitumwa kutoka nchini Rwanda kwa
wapangaji waliotoka kwenye jeshi la Burundi.
Nyamitwe
alivamiwa alipokuwa akirudi nyumbani mwake Magharibi mwa Kajaga huko
Burundi lakini si mara ya kwanza kupatwa na tukio kama hilo.
Mwezi Julai mwaka huu Burundi iliishtumu Rwanda kwa mauaji ya Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Hafsa Mossi aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura.
Mwezi Julai mwaka huu Burundi iliishtumu Rwanda kwa mauaji ya Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Hafsa Mossi aliyeuawa kwa kupigwa risasi mjini Bujumbura.
0 comments:
Post a Comment