Karagwe-Kagera
Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso akiwa wilayani Karagwe Mkoani Kagera amewakabidhi wakandarasi M/s Afcons Infrastructure Limited and Vijeta Projects and Infrastructures Rwakajunju kwenda Mji wa Kayanga Karagwe wenye gharama ya Dola za Marekani Milioni 27.963 (sawa na shilingi bilioni 64.32).
Akikabidhi mradi huo Waziri Aweso amesema ana imani na Mkandarasi huyu na ameagiza Mkandarasi kutekeleza mradi huo kwa ubora na kwa muda mfupi ili adhma ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani inafikiwa kwa wakati.
Aidha Mhe Aweso katika ziara yake Wilayani Karagwe, amezindua mradi wa Maji wa Ahakishaka wenye thamani zaidi ya Sh Milioni 670 unaokwenda kuhudumia wananchi zaidi ya 2,500 wa Kijiji cha Ahakishaka Wilayani Karagwe
Akitoa taarifa ya mradi huo Mhandisi Cassian Wittike ambae ni Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Karagwe, ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayo ongozwa na Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za kutekeleza mradi huu ambao umekua mkombozi kwa wananchi ambao walikua wamepata adha ya maji kwa muda mrefu ikiwemo kununua maji kwa sh 1,000 kwa ndoo ya lita 20 na sasa rasmi watalata huduma hiyo kwa sh.30 kwani mradi unatumia nishati ya solar.
0 comments:
Post a Comment