Na Mathias Canal, Ushetu-Shinyanga
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Mwaka 2023 Ndg Abdalla Shaibu Kaim amempongeza Mkuu wa Wilaya ya Kahama Mhe Mboni Mhita, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ushetu Bi Hadija Mohamed Kabojela, Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe Dkt Emmanuel Cherehani, Madiwani na watumishi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu kwa miradi yote kupitishwa na Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza wakati wa makabidhiano ya Mwenge huo wa Uhuru mwaka 2023 kutoka Halmashauri ya Ushetu kwenda katika Halmashauri ya Wilaya ya Msalala kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa amesema kuwa Halmashauri ya Ushetu inapaswa kupongezwa kwani imetekeleza miradi yake kwa umakini, weledi na viwango vikubwa.
Amesema kuwa Halmashauri ya Ushetu inapaswa kuigwa kwani miradi yake ya maendeleo iliyopitiwa na Mwenge wa uhuru ipo katika ubora wa hali ya juu na utekelezaji wake unafanyika ndani ya muda uliokusudiwa.
Ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilometa 99, Katika tarafa 02, Kata 08, Vijiji 21 na kupitia jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 920,239,148.91.
Mwenge huo wa uhuru umeweka mawe ya msingi miradi 03 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 345,405,000.00 sambamba na kuzindua mradi 01 wenye thamani ya Shilingi Bilioni 229,750,088.91, umefungua mradi mmoja wenye thamani ya Shilingi Bilioni 101,500,000.00 na kukagua mradi 01wenye thamani ya Shilingi 243,534,060.00. Kadhalika Mwenge umeona kwa vitendo shughuli za Mapambano dhidi ya Virusi vya UKIMWI na UKIMWI, Mapambano dhidi ya Malaria, Lishe, Mapambano dhidi ya Rushwa, Madawa ya Kulevya na Shughuli za upandaji wa miti.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment