Wawekezaji wa ndani wanao taka kujenga
viwanda vya dawa wahimizwa kuhakikisha wanakidhi vigezo vya uzalishaji
wa dawa ili kuweza kuruhusiwa kufanya shughuli hiyo ya uzalishaji wa
dawa.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati
akizindua maabara hamishika zakudhibiti ubora na usalama wa dawa mapema
leo katika viunga vya mamlaka ya dawa, chakula na Vipodozi (TFDA)
Aidha Mh. Ummy ameahidi kuongeza
jitihada za kudhibiti ubora, usalama, na ufanisi wa bidhaa hasa dawa kwa
kuimarisha mpango mahususi wa uchunguzi wa awali wa Dawa mbao ulianza
2002 unaohusu uchunguzi wa Dawa muhimu za Kifua kikuu, Dawa za ARV, Dawa
za Maleria pamoja na Viuwa sumu.
Kwa upande mwingine Mh. Ummy
amesisitiza athari za uwepo wa dawa zisizo na ubora katika jamii ikiwepo
kuhathiri uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na taifa kiujumla kutokana
na kmanunuzi ya Dawa zisizo na uwezo wa uwezo wa kutibu mwisho
hupelekea usugu wa Dawa katika mwili.
Waziri Ummy hakusita kuipongeza Bodi ,
Uongozi na wafanyakazi wa TFDA kwa utendaji mzuri wa kazi huku
akiahidi kuendelea mkuwaunga mkono kwa kushirikiana nao kwa ukaribu
katika safari ya kumsaidia Raisi wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John
Magufuli.
Nae Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo alisema kuwa kutokana na
kuongezeka kwa Maabara hamishika itasaidia kuwabaini na kuwakamata
wahalifu wanaofanya biashara hiyo ambayo inahathiri jamii na uchumi
kiujumla.
“Mwaka 2005 wastani wa dawa bandia
ulikuwa 3.7 wa dawa zilizokuwepo huku takwimu za 2017 imeshuka kwa
chini ya 1%” , alisema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na
Vipodozi (TFDA) Hiiti Sillo, huku akisema mafanikio hayo yanatokana na
ufuatiliaji wa umakini unaofanywa na taasisi hiyo.
Bw. Hiiti Siilo aliendelea kwa kusema
kwamba katika utekelezaji wa majukumu yake TFDA imepanga kupeleka
maabara hizo katika ofisi za kanda ambazo hazikuwa na huduma hiyo
ikiwemo ofisi ya Tabora, Hospitali ya Mbeya na Mtwara huku nyingine
zitapelekwa katika vituo vya Forodha Namanga,KIA mpakani, Silali
(Tarime) na Mutukula (Kagera) bila kusahau Geita na Katavi, alisisitiza
Bw. Sillo
0 comments:
Post a Comment